April 23, 2018Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wa Mashindano, Hussein Nyika, umesema kuwa umekata rufaa TFF kulalamikia mchezaji mmoja wa Mbeya City kuzidi Uwanjani.

Nyika ameeleza kuwa wametuma malalamiko hayo kufuatia mchezaji wa Mbeya City kuonekana Uwanjani wakiwa 11 badala ya 10 wakati mmoja wao alikuwa ameshapewa kadi nyekundu.

Yanga wamefikia hatua ya kufanya hivyo baada ya beki wa Mbeya City, Ramadhan Malima kupewa kadi nyekundu, na kisha baadaye kuonekana tena Uwanjani wakati zikiwa zimebakia dakika takribani 6 mchezo kumalizika.

Wakati mechi hiyo ikielekea mwisho, Kocha Msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa, alionekana akibishana na Kamisaa wa mchezo huo, kuhoji kwanini Mbeya City wapo 11 badala ya 10.

Nsanjigwa alionekana akiwa amepandisha munkari akitaka kujua kipi kilichosababisha mpaka aendelee kusalia Uwanjani wakati kanuni haziruhusu.

Mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, ilimalizika kwa sare ya 1-1, Yanga wakifunga kupitia Rafael Daud na Mbeya City kupitia Iddy Naddo.


6 COMMENTS:

 1. Hujatuambia kuhusu vijana wetu huko congo jana ilikuaje?

  ReplyDelete
 2. Dah!
  Sasa Yanga wanaanza kupoteza muelekeo. Wanaanza kulilia ushindi wa mezani Huyo mchezaji aliepewa kadi nyekundu kuonekana uwanjani anamahusiano gani na matokeo ya uwanjani? Kama wa kukata rufaa walikuwa Mbeya City kwa kuwa Yanga walibebwa na ile kadi nyekundu. Sasa Yanga wanamkatia nani rufaa Mbeya City au wanakata rufaa wasimamizi wa mchezo kwa kutomundosha huyo mchezaji uwanjani?

  ReplyDelete
 3. hapa kinachotakiwa ni kithibitisho kama mbeya city baada ya kutolewa mchezaji wao na kubaki kumi je ni kweli baadae wakacheza kumi na moja ???
  video zipo na kila mtu kaona haina haja kubishana hapa !!

  ReplyDelete
  Replies
  1. Vyovyote itakavyokuwa hakuna points za mezani. Makosa ya muamuzi hayawezi kuiathiri timu....

   Delete
 4. Soka la Tanzania pasua kichwani,yaani mshabiki anataka kujadili kitendo kama hicho kweli!!!

  ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV