April 27, 2018



Taarifa zinaeleza kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre, amekuwa miongoni mwa Makocha 77 waliotuma maombi ya kazi nchini Cameroon.

Lechantre ambaye amejiunga na Simba kuchukua mikoba ya Mcameroon Joseph Omog, ametuma maombi ya kuomba nafasi ya kuifundisha timu ya taifa ya Cameroon huku akikumbana na mchuano mkali.

Cameroon ipo katika msako wa kocha mpya ili kuchukua nafasi ya Hugo Broos aliyefungashiwa virago mwishoni mwa mwaka jana.

Inaelezwa pia Mcameroon wa zamani wa Simba, Joseph Omog, ni moja ya Makocha waliotuma maombi ya kukinoa kikosi hicho cha Cameroon, maarufu kama Indomitable Lions.

Kocha wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet naye ametuma maombi ya kupata kibarua cha kuifundisha timu hiyo.

Uwepo wa Makocha hao unafanya mchuano wa kupata kazi ya kuinoa Cameroon kuwa mgumu kwa Lechantre, kutokana na asilimia ya wengi kuwa na CV's nzuri.

Mfaransa wa Simba ametuma maombi hayo akiwa anakiandaa kikosi chake kuelekea mechi dhidi ya watani wa jadi, Yanga, itakayopigwa Arpili 29 katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic