April 1, 2018




Na Saleh Ally
HIVI karibuni nilifunga safari kwenda Afrika Kusini, mahsusi kumfanyia mahojiano beki wa Baroka FC, Abdi Banda.


Huyu ni kijana wa Kitanzania ambaye anacheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini. Banda amepita Coastal Union na baadaye Simba kabla ya kupata timu.

Kila mmoja wetu anajua kwamba sasa Banda ni hazina ya taifa kwa kuwa ni beki wa kati tegemeo wa kikosi chetu cha timu ya taifa akishirikiana na mkongwe, Kelvin Yondani.

Katika mahojiano naye, kama ilivyo ada ya Banda ni muwazi, si muoga na mwepesi kusema kile anachoona anastahili kukisema.

Katika moja ya mambo aliyoelezea wakati akijibu maswali ya Global TV Online na Championi, ni pale alipoeleza namna anavyokerwa na viongozi wa mpira wa Tanzania kuzungumzia mambo ya waamuzi kwenye mikutano ya waandishi wa habari.



Banda alieleza namna alivyokerwa na kuona kiongozi wa soka nchini alipoitisha mkutano wa waandishi wa habari na kulalamika mwamuzi kutoipa timu yake penalti wakati ilistahili kupata.



Ingawa umepita muda, lakini siku chache zilizopita, Msemaji wa Simba, Haji Manara alionekana kukerwa na kauli ya Banda. Huenda aliamini alikuwa akimshambulia, naye akajibu kadiri ya uwezo wake akionyesha kutokubaliana na kilichoelezwa.


Hawa wawili, ni watu tofauti kwa mambo mengi sana. Banda ni mchezaji aliyekuwa akitoa maoni yake na kile alichojifunza Afrika Kusini tofauti na mpira wa Tanzania. Manara naye ni msemaji wa Simba ambaye hajawahi kucheza Afrika Kusini, Tanzania au nje ya Tanzania.

Kila mmoja ana maoni kulingana na anachokiona sawa na Manara hakumtukana Banda licha ya kuonyesha kukerwa na kile ambacho Banda alikijibu katika mahojiano hayo ya Global TV Online na gazeti hili la Championi.



Baada ya hapo, hakika nilishangazwa sana na kuona watu mbalimbali kwenye mitandao wakivurumisha matusi rundo kwa mchezaji huyo na wengi wakizungumza vitu ambavyo vinaonyesha wazi ilikuwa ni chuki.

Mfano wako waliosema anajiona, kucheza Afrika Kusini kashafika, Afrika Kusini si lolote, anajiona mzuri sana. Ana mbwembwe, anaringa na kadhalika.



Hata Manara alipotoa hoja zake akionyesha alikuwa na povu lake, lakini hakuwa ameweka hata tusi moja kumtukana Banda. Wale wanaotukana wametokea wapi na kwa nini wafanye hivyo?



Kuna sababu ya kujifunza na wakati mwingine kuachana na ubinafsi badala yake kuthamini sana utu wa mwenzako pia.



Kama una wivu, Banda ana kitu wewe hauna basi tafuta kama unaweza kukipata badala ya kitu hicho kukujaza hasira na kutukana bila ya sababu. Uzuri wake ni ishu? Kujizungumzia vizuri kwa hatua aliyofikia ni jambo baya? Kuzungumza maoni yake kutokana na alichojifunza ambacho hukijui ni ubaya?



Kama wewe haujacheza Afrika Kusini, unajuaje hilo. Kama kweli Afrika Kusini hawalaumu waamuzi kwa kuwa wanajua yalishapita, kwa nini unakataa au kwa nini unakasirika?



Banda na Manara nani anajua zaidi vitu vya Afrika Kusini? Na kama wewe au kuna watu wanalaumu kwamba kwa sasa, kuna shida ya uhuru wa kujieleza, vipi sasa na wewe unazuia watu kuwa huru kujieleza mambo wanayoyajua au wanayoyaamini?

Pia nahoji kwa kila aliyetukana, hivi kutukana ndiyo akili? Kusema maneno ya matusi ndiyo utaalamu?


Binafsi naona wenye matusi katika suala la hoja ya uchanganuzi kuonyesha Banda alikuwa sahihi, au Manara ndiye alikuwa sahihi ni ukosefu wa hoja za msingi.


Yaani watu ambao hukosa hoja za msingi, basi hukimbilia kutukana. Au watu ambao wanachukizwa na maendeleo ya wenzao wakati wao wakiwa wavivu na wamelala ndiyo hukimbilia matusi.

Tuache chuki kwa kuwa hakuna aliyewahi kufanikiwa kupitia chuki. Kutukana kwa kuwa unaumizwa na mafanikio ya mwingine, hakuwezi kukusaidia badala yake utaendelea tu kujiumiza.


Kama unaona Banda amekosea, weka hoja mezani. Ndiyo maana kuna wale wanaojitambua ambao wameonyesha wapi Banda amekosea na wengine wakaeleza ukweli aliosema wakimtaka Manara kuuchukua badala ya kuendelea kulalamika.

Huna hoja, basi nyamaza. Matusi hayawezi kuonyesha unajitambua, yanakushushia hadhi na heshima na pia tuheshimu uhuru wa watu kujieleza na vizuri kuyapinga maelezo yao kupitia hoja badala ya chuki na matusi kwa kuwa mnakuwa nje ya hoja husika.

Nawakumbusha mwishoni, Banda ni mchezaji wa timu yetu ya taifa, ni kijana mdogo kuliko mnavyofikiria. Tuonyesheni upendo kwa Watanzania wenzetu, tuvumiliane na kukosoana kwa misingi badala ya kutanguliza chuki na ubinafsi. Tuikimbie dhambi ya chuki.





11 COMMENTS:

  1. Mnashangaza sana. Hivi Manara kulalamikia Refa yeye ni wa kwanza? cha kumchukiza Banda ni kipi kama si kuonyesha kasoro zake alizonazo? Inawezekana malezi mabaya. Haji Manara anao wajibu wa kuzungumza kwa kuitetea klabu yake. Kwanini Banda kimkasirishe? Wewe mwandishi msaidie mchezaji huyu kufikiri na kutambua mipaka ya kila mmoja yeye kama mchezaji na Manara kama kiongozi na msemaji wa klabu yake badala ya kumvimbisha kichwa kwa kuongea pasipo mipaka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi ndugu yangu unadahni kitengo cha babari bakipo katika club za wenzetu walioendelea? Hivi ni lini uluwahi kuwasikia Mkuu wa kitengo cha habari arsenal au chealsea au man u akizungumza habari za ufundi au kasoro za mwamuzi kwenye press conference tena akiwa Na TV ya kuonesha ushahidi? Kama huko ulaya ni mbali sana hivi ulishawahi kumwona Mkuu wa kitengo cha habari wa club ya TP mazembe akijitokeza kuongea au kufanya yale yafanywayo Na wakuu wa idara ya habari qa club zetu? Nini maana ya weledi? Kwanini tunakumbatia maovu kwakuzidiwa Na unazi? Hivi anachofanya Haji Manara ni sahihi kwa wakati huu tulionao? Hivi kuwasema vibaya kwenye mitandao ya kijamii wachezaji wa timu pinzani ndio professionalism? Haji anapaswa kushajiisha naendelea ya soka letu kisasa Na si kama afanyavyo mambo mengine yanatia aibu soka letu

      Delete
    2. what are you talking about?????? Unajua usemacho wewe??? Wenzetu Manager wa timu ndiye huzungumzia chochote kuhusu mechi hasa anapokuwa ktk Press Confernece. Wakati Arsene Wenger anawaita waamuzi wa Uingereza 'untouchable' ilikuwa nawasifia au anawalalmikia? Mara ngapi wachezaji na makocha wanaathibiwa kwa kuwasumbua marefa? Uwe makini unapokuwa unaonge jambo

      Delete
  2. Manara ni msemaji wa club na nadhani ni wajibu wake kuzungumzia mambo yanaihusu club yake bila ya aibu au woga wowote ule. Na cha ajabu na ujinga wetu sisi watanzania ni kwamba Khaji Manara anachokipigania ni maboresho ya waamuzi wetu wawe watajitahidi kuzingatia maamuzi bora wanapokuwa mchezoni. Sasa kosa la Khaji Manara liko wapi hapo? Yeye Banda yupo Africa Kusini kama atakuwa na kumbu kumbu nzuri atakumbuka yakuwa mchezo kati ya Afrika Kusini na Senegal ilibidi urejewe na kuchezwa tena upya baada ya Senegal kumlalamikia Referee kuwa maamuzi yake yalikuwa na utata. Na kweli baada ya malalamiko yale ya wasanegal kufuatiliwa ikagundulika kuwa kweli Referee kwa namna moja au nyengine alitoa maamuzi ya kuibeba Africa kusini na kupelekea Referee yule wa Ghana kufungiwa maisha na FIFA. Hapa kwetu licha ya malalamiko yote yanayotolewa na wadau wa soka kuhusu uamuzi m'bovu unaotolewa na waamuzi wetu lakini la kushangaza bado kuna watu wanawatetea waendelee na upuuzi wanaoufanya. Hii ndio Tanzania na Referee akeshaamua kitu ndio kimepita hata kama kina uhalali wote wa kuhojiwa na mtu kama Manara akihoji anaonekana mkorofi na la kushangaza zaidi wanamuona mkorofi ni vijana wetu wanaojinasibu kuwa wamepiga hatua kisoka sasa we acha tu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. umenena vema sema watanzania wana visokorokwinyo kwa kuwa tu kaongea wa upande mwingine. Sasa sijui kizuri gani Banda alichofanya hadi huyu mwadishi anaona kaonewa na wanaomjibu

      Delete
  3. Saleh Jembe naona naanza kuwa na wasiwasi wako juu ya kuyatafakari mambo. Kimsingi huna haja ya kuwanyooshea vidole watu na wala hakuna aliyemtukana kama unavyotumia njia hiyo kuharamisha upuuzi wa Banda. Kama professional Player anapaswa kujua ni lipi a kuzungumza na lipi si la kuzungumza. Unaposema ati ni msema ukweli na muwazi ala hamuogopi mtu, unamaanisha nini? Ulimhoji mwenyewe, kama kweli uko fair ebu tafakari swali ulilomuuliza na jibu alilolitoa vinaendana? Ni jibu la kutolewa na mchezaji kama yeye? Kwanza alijibu tukio ambalo hata yeye halikumtokea wala hakuwepo. Kwanini asingesema kuwa hapendi kimtokee kitendo cha kumpiga mchezaji wa Kagera ambacho ni utovu wa nidhmu? Kumna kosa na dhambi gani mtu kulalamikia uozo wa refa? Yeye awapo uwanjani mboni huwa analalamika Alikuwa na yake moyoni, sasa wale wanaojua hawawezi kumwachia tu kisa uhuru wa kuzungumza.

    ReplyDelete
  4. sio kila mnachosema au kuandika ni sahihi kwani nyie mnaomsifia banda ndio nyie nyie mliomsema wakati anamshambulia mchezaji wa kagera, nani hajui ubovu wa waamuzi wa Tanzania mbona juzijuzi CAF wamesimamisha waamuzi wa Tanzania kwa tuhuma za rushwa

    ReplyDelete
  5. mimi naona yeye ndo alitumia vibaya uhuru wa kujieleza maana anaulizwa hiki anajibu kile na ameandamwa as professional player kuna muda anatakiwa akae na kuangalia interview za kaka zake hasa captain wetu Mbwana Samatta mfano aliulizwa kuhusu mashabiki wa Tz namna wanavoshabikia pale tu timu ikipata matokeo chanya akasema ye kazi yake mpira mashabiki ni motisha tu wao kinachotakiwa ni wacheze mpira na kuhusu kocha akasema hana comment ingekuwa ni yeye huyu angejibu nini ktk hilo mie naona hajakosea kwa sababu hajavunja sheria but atambue mipaka ya kujieleza kuna underground wengi inabidi wajifunze mambo mengi kutoka kwake na wanaamini anakitu cha kuwafunza lakini kwa response yake it was two things which are partly different labda ingekuwa kutoka kwa wachezaji wa mchangani may be tungechukulia poa mind him tuache ushabiki that Baroka Fc he is still having long journey to go if truly he needs to reach far but akiweka majungu mbele hawezi jua kesho yake atakuwa wapi any way but may be it is bcoz of the nature acha tuache

    ReplyDelete
  6. Tatizo lako Saleh jembe ni unazi wa Yanga wa kupitiliza toka Banda anaenda south imekua nongwa . Mara anafanyiwa fagisu na Viongozi mara ananyimwa kibali ili mradi upate cha kuichonganisha simba. Sasa mbona hamtuambii timu ya abdi
    Banda inashika nafasi ya ngapi kwenye league?

    ReplyDelete
  7. Toeni Mapovu tu!! Banda mwanangu watakukuta wapi? Chunga wasikuundie wasiojulikana kwa sababu nchi hii hatari sana.

    ReplyDelete
  8. Nafikiria hata kuliacha kulisoma gazeti hili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic