Na George Mganga
Walikuwa ni Yanga walioanza kupata bao la kwanza kupitia Rafael Daud mnamo dakika ya 57 baada ya kumalizia vema mpira wa adhabu na kuandika bao hilo.
Mbeya City walimka na kuanza kutafuta bao la kusawazisha, lakini walipatwa na pigo kwa beki wake, Ramadhani Malima kutolewa nje kwa kadi nyekundu na kubaki 10 Uwanjani.
Katika dakika ya 93 zikiwa zimeongezwa 6 mpira kumalizika, Mbeya City walipata bao la kusawazisha kupitia kwa Iddy Naddo aliyefunga kwa kichwa kufuatia krosi safi iliyopigwa upande wa kulia mwa Uwanja.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga ijipatie alama moja pamoja na Mbeya City, ambapo sasa imefikisha alama 48 kwenye msimamo huku watani zake wa jadi Simba wakiwa na 59.
0 COMMENTS:
Post a Comment