April 22, 2018



Na Mpiraaa umekwishaaa, dakika 90 zimemalizika katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, Mbeya City 1-1 Yanga

Dak ya 98, Mpira unaendelea huku dakika ambazo zimeongezwa zikiwa zimemalizika
Dak ya 97, Mpira unarushwa kuelekea langoni mwa Yanga
Dak ya 95, Muda si mrefu mpira utamalizika
Dak ya 92, Mbeya City wanaamka sasa, wanakwenda langoni mwa Yanga lakini mpira unaokolewa

DAKIKA SITA ZIMEONGEZWA

Dak ya 90, Gooooooli, Mbeya City wanachomoa, Iddy Naddo anafanya matokeo kuwa 1-1
Dak ya 89, Goli Kiki, mpira unapigwa kwenda Yanga

Dak ya 88, Mhilu amedondoka chini, machela imeingizwa ndani ya Uwanja kumbeba
Dak ya 86, Cannavaro anapewa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu mchezaji wa Mbeya City
Dak ya 85, Yanga wanapanda na mpira kuelekea langoni mwa City, Chirwa anapoteza na wanaokoa
Dak ya 83, Mchezaji Juma Abdul kaumizwa, ni faulo kuelekea Mbeya City
Dak ya 83, Mbeya wanapambana wakijaribu kusaka bao la kusawazisha, lakini Yanga wamekuwa imara eneo la ulinzi

Dak ya 82, Mbeya City wanapata kona, inapigwa na kuokolewa na mabeki wa Yanga
Dak ya 80, Yanga wanapata nafasi ya kuongea bao la pili, Chirwa anashindwa kuitumia vizuri nafasi
Dak ya 79, Kona inapigwa japo Ngome ya Mbeya City inakuwa imara inaokoa mpira
Dak ya 78, Mwasapili anatoa mpira nje, unarushwa kuelekea Mbeya City, unarushwa lakini unatolewa tena inakuwa kona
Dak ya 77, Ni goli kiki kwa Yanga, mpira unapigwa kuelekea Mbeya City
Dak ya 75, Tayari Mbeya wameshaanza, wanakwenda kushoto mwa Uwanja, namnagani mpira unakwenda nje, 
Dak ya 74, Faulo inapigwa kuelekea Yanga, mabeki Mbeya City wanaokoa

Dak ya 71, Mpira umeshaanza baada ya utulivu kuonekana Uwanjani
Dak ya 70, Mpira bado umesimama Uwanjani sababu ya vurugu, mawe yalirushwa
Dak ya 67, Mpira umesimama, vurugu zimetokea Uwanjani
Dak ya 64, Nafasi nyingine kwa Yanga, faulo nyingine, na kadi nyekundu inatoka kwa mchezaji wa Mbeya City
Dak ya 63, Tayari mpira umeanza tena, ni faulo inapigwa kueleka Yanga, kipa Chaima amepiga mbele na kuwafikia mabeki wa Yanga, wanautoa nje, tayari usharushwa 

Dak ya 61, Vurugu zinatokea uwanjani, mashabiki wa Mbeya City wanarusha chupa

Dak ya 60, Mpira unarushwa kuelekea Mbeya City,
Dak ya 58, Faulo nyingine kwenda Mbeya City, Yanga wamemka kwa kasi kubwa
Dak ya 57, Inapigwa huku kwake Rafael Daud, goooooooli, Yanga wanapata bao la kwanza
Dak ya 55, Mwasapili anapewa kadi ya njano kwa kucheza faulo. Juma Mahadhi anafanyiwa madhambi

Dak ya 54, Chirwa amepata kadi ya njano, ataukosa mchezo ujao dhidi ya Simba baada ya kufikisha idadi ya kadi tatuDak ya 53, Ramadhani Malima yuko chini ameumia, mpira umesimama, madaktari wanaingia Uwanjani kumganga
Dak ya 53, Chirwa anatoa mpira nje, unarushwa kuelekea Yanga
Dak ya 51, Martin anatoka na nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi
Dak ya 51, Mhilu anakuwa hana bahati leo, mpira unamkataa

Dak ya 50, Mpira unatoka nje, na harakaharaka Yanga wanarusha
Dak ya 49, Faulo inapigwa kwenda Mbeya City baada ya Chirwa kufanyiwa madhambi
Dak ya 48, Kocha Mbeya City anapaza sauti kutoa maelekezo kwa wachezaji wake, mambo yamekuwa magumu
Dak ya 47, Gadiel anarusha mpira baada ya Mbeya kuutoa
Dak ya 45, Yusuph Mhilu anakosa nafasi ya kumalizia krosi safi ya Emmanuel Martin, ni kipindi cha pili sasa

Mapumziko: Kipindi cha kwanza kimekwisha

Dak ya 46, Umepigwa na Yanga wanaondosha mashambulizi, Faulo inatokea nje kidogo mwa 18 ya Mbeya City. Inapigwa chinichini lakini kipa Chaima anadaka
Dak ya 45, Faulo kuelekezwa Yanga, hangaya amechezewa madhambi

DAKIKA MBILI ZIMEONGEZWA KUELEKEA MAPUMZIKO

Dak ya 44, Mhilu anafanyiwa madhambi, Makomandoo wa Yanga wanamtupia lawama Mwamuzi
Dak ya 44, Ikobela anachezwa tena madhambi, inakuwa faulo, pigwa mbele huku, Rostand anakuwa imara anadaka mpira
Dak ya 42, Ninja anapasiana na Yondani, kwake Chirwa, inakuwa faida kwa Mbeya City baada ya mchezaji kuchezewa faulo, mpira unaelekezwa Yanga
Dak ya 41, Dakika zinazidi kuyoyoma huku milango ikiwa migumu kufungika

Dak ya 39, Ramadhani Malima anapewa kadi ya njano baada ya kucheza madhambi, ni faulo, inapigwa huku lakini kipa Owen Chaima anadaka
Dak ya 38, Yanga wanshindwa kujipanga vema baada ya kupata nafasi nzuri tena ya kutengeneza bao, Buswita anashindwa kuuhimili mpira
Dak ya 38, Mpira unaanza tena, Rostand anapiga mbele
Dak ya 36, Kona ya tatu kwa Mbeya City, inapigwa huku lakini msala unamwangukia Yondani baada ya kuchezewa faulo na Victor Hangaya, Mwamuzi anampa kadi ya njano

Dak ya 35, Mpira upo katikati mwa Uwanja, Ninja anachezewa madhambi, inakuwa faulo
Dak ya 34, Ni faulo tena kuelekezwa Yanga, baada ya mchezaji Mbeya City kuchezewa madhambi
Dak ya 32, Frank Ikoble anang'aa Uwanja wa Sokoine, anaufanya mpira anavyotaka
Dak ya 30, Ni goli kiki kwa Yanga, Rostand anaanzisha mpira, unapigwa kwenda mbele na Mbeya wanaunyakua tena, unarushwa kuelekea Yanga
Dak ya 29, Milango bado ni migumu kufungika mpaka sasa

Dak 28, Yanga wanapandisha mashambulizi kuelekea langoni mwa Mbeya, pigwa krosi kuubwa na kwenda nje moja kwa moja
Dak ya 26, Goli Kiki, Mbeya City wanaanza, makapu anamchezea rafu Ikobela, mpira unapigwa kwenda Yanga, anao Mhoammed Samatta, piga krosi huku, Yanga wanautoa nje
Dak 25, Anapiga Rafael Daud lakini hesabu zake hazijawa nzuri na mpira unakwenda nje
Dak ya 24, Mpira wa kurushwa kwenda Yanga, anarusha Juma Abdul, kwake Emmanuel Martin, ni faulo kwenda Mbeya City, anaonekana Gadiel na Rafael wakitaka kupiga

Dak ya 22, Mpira upo langoni mwa Yanga, wanauchukua Mbeya City Dak ya 20, Kipa wa Mbeya City anaanzisha mpira kwa kupiga mbele, hatariiii, imepigwa moja ndefu huku lakini inagonga mtambaa panya
Dak ya 20, Kuliwa mwa Uwanja huku Yanga wanasonga, ni offside tena
Dak ya 19, Yondani anaanza tena kucheza mpira wa adhabu, anaanza na kipa Rostand, piga katikati kumsaka Ninja
Dak ya 18, Yanga wanapandisha tena mashambulizi mbele, Mhilu anajaribu kutengeneza nafasi huku, offside

Dak ya 17, Mpira sasa upo katikati ya Uwanja, kwake Chirwaaa, namna gani pale anakutana na kipa anaokoa mpira, ilikuwa nafasi nzuri kwa Chirwa kupachika bao
Dak ya 16, Yanga wanaonekana kulisakama lango la Mbeya kwa udi na uvumba kusaka bao la mapema
Dak ya 13, Mpira umesimama, Yondani anagangwa
Dak ya 13, Juma Abdul anarusha mpira kuelekea Mbeya, Yondani anachezewa madhambi na Ikobela, faulo kuelekea Mbeya

Dak ya 11, Kona inapigwa kuelekea Mbeya, Yondani ametoa nje, pigwa huku Buswita anaokoa
Dak ya 9, Faulo inapigwa na Samatta karibu na eneo la kupigia kona lakini inakuwa kubwa na kwenda nje, ni goli kiki
Dak ya 8, Mpira umeshaanza, Mbeya wanapiga kuelekeza mbele, Ikobela anchezewa madhambi, mpira unaelekezwa Yanga
Dak ya 8, Baadhi ya mashabiki wasio na viingilio wamepanda juu ya miti wakitazama mpira
Dak ya 7, Mchezaji Mbeya City ameumia, mpira umesimama kwa muda

Dak ya 5, Kevin Yondan anafanya jitihada za kuokoa shambulizi hatari la Mbeya City, ilikuwa ni nafasi kwao kuandika bao la kwanza
Dak ya 5, Mpira mwingine wa adhabu unapigwa kuelekea Mbeya City, anapiga Juma Abdul, amepiga lakini mabeki wanaokoa
Dak ya 4, Gadiel Michael anachezewa faulo, mpira unapigwa kuelekea Mbeya City
Dak ya 3, Mpira umeshaanza Uwanja wa Sokoine, Mbeya

2 COMMENTS:

  1. Mtapigwa tu,lazima mpigwe,maana hakuna namna.

    ReplyDelete
  2. Leo nimefurahi..maana jana kulikuwa hakuna live stream ya Simba Vs Lipuli...sijui muandishi alipigwa ganzi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic