April 4, 2018




Na George Mganga

Baada ya uwepo wa taarifa zilizozagaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuwa uongozi wa Azam FC umefuta cheo cha Afisa Mtendaji wa timu hiyo, Afisa Habari wa klabu, Jaffer Idd Maganga, amekanusha taarifa hizo.

Jaffar amekanusha uvumi wa taarifa hizo kuhusu kufutwa kwa cheo hicho huku akieleza kuwa kama suala hilo litatokea basi taarifa rasmi itatoka.

"Hakuna ukweli wa taarifa hizo, jambo lolote likitokea ndani ya Azam, klabu itatoa taarifa rasmi" alisema Maganga.

Taarifa zilizo chini ya kapeti zinaeleza kuwa cheo hicho cha Afisa Mkuu Mtendaji wa Azam FC ambacho kipo chini ya Abdul Mohammed, kimeshaondolewa na badala yake Mohammed atapangiwa majukumu mengine ya kufanya ndani ya klabu.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic