April 14, 2018



Taarifa kwa Umma

Habarini za jumaamosi wadau wote wa soka wa mkoa wa Ruvuma hususani wa Songea Mjini.

Ikumbukwe Mbunge wa jimbo la Songea Mjini Daktari wa Sheria Damas Daniel Ndumbaro alipokua kwenye harakati zake za kuhakikisha kuwa timu ya Majimaji inafanya vizuri alitoa ahadi ya kuwapa wachezaji wa timu hiyo kiasi cha shilingi milioni tano (5,000,000/=) za kitanzania kama motisha kwa wachezaji kwa kila mchezo watakaoshinda.

Katika kutekeleza ahadi yake hiyo ya kizalendo kabisa kwa timu yetu pendwa ya Majimaji tayari Mbunge wa jimbo la Songea Mjini Dkt. Damas Daniel Ndumbaro amekwisha wakabidhi viongozi walioko na msafara wa timu yetu kiasi hicho cha pesa.

Dkt. Ndumbaro amesema ataendelea kutoa kiasi hicho cha pesa kwa kila mechi ambayo timu hiyo itapata ushindi kama motisha kwa wachezaji hao kama alivyoahidi kwakua lengo na tamaa yake yeye kama Mbunge wa jimbo hili ni kuiona Majimaji ikifanya vizuri na kusalia kwenye ligi kuu msimu huu.

Dkt. Ndumbaro amesisitiza kua uwepo wa timu ya Majimaji kwenye ligi ni jambo kubwa na jema kwa uchumi wa Mkoa wa Ruvuma hususani Manispaa ya Songea kutokana na timu hiyo kusababisha ujio wa wageni wengi wanaokuja kutazama michezo mbalimbali inayochezwa kwenye dimba la Majimaji.

Aidha Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuendeleza umoja na mshikamano ndani na nje ya timu ya Majimaji kwani hiyo ndio njia pekee itakayoweza kuinusuru timu hiyo kushuka daraja msimu huu.

Mwisho Dkt. Ndumbaro amewasihi wana Songea kutokukata tamaa bado timu ya Majimaji ina nafasi ya kusalia kwenye ligi kuu endapo nguvu za wanamichezo wote zikiunganishwa pamoja.

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano.
Ofisi ya Mbunge.
Jimbo la Songea Mjini.
14/04/2018

1 COMMENTS:

  1. Dr, motisha ni sehemu tu itayoleta ushindi, lakini kuna mengi sana mengine yanayohitajika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic