April 2, 2018




Vurugu ziliibuka baada ya Sin­gida United kufanikiwa kuwatoa Yanga katika robo fainali ya Kombe la FA jana Jumapili.

Kocha wa Singida, ambaye aliwahi kuinoa Yanga, Hans van Der Pluijm, baada ya ushindi huo wa penalti jana, alijaribu kwenda kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Yanga ili kuwapongeza lakini akakutana na kizuizi cha ma­komandoo wa timu hiyo waliod­hani kuwa anakwenda kuwabeza, walipomtaiti na kumzuia alikasiri­ka na kurusha ngumi hewani.

Hata hivyo, askari waliokuwa karibu waliibuka na kuamua ugomvi huo, huku wakimuondoa kocha huyo na kuacha majibizano baina ya viongozi wa Yanga na wale wa Singida United.
Singida United imefanikiwa kutinga nusu fainali baada ya kuifunga Yanga kwa penalti 4-2 kufuatia sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Namfua mjini hapa.

Singida imeungana na Stand United, Mtibwa Sugar na JKT Tanzania kucheza hatua ya nusu fainali ya Kombe la FA.

Singida itavaana na JKT Tanza­nia kwenye Uwanja wa Namfua, wakati Mtibwa itaumana na Stand United kwenye Uwanja wa Manungu.

Katika mchezo wa jana, Singida United inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga, Hans van Der Pluijm ilionekana kucheza kwa malengo zaidi lakini hali ya uwanja kujaa maji kutokana na mvua iliyoanza kunyesha wakati timu zikiingia uwanjani, iliharibu mipango yao mingi.

Yanga ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 23 lililofungwa kwa kichwa na Yusuph Mhilu akiunganisha kona iliyopigwa na Ibrahim Ajibu akiwazidi ujanja mabeki wa Singida United.
Singida United ilisawazisha bao hilo dakika ya 46 kupitia kwa Kenny Ally baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Yanga.

Katika penalti, waliokosa kwa Yanga ni Papy Kabamba Tsh­ishimbi na Emmanuel Martin huku Gadiel Michael na Kelvin Yondani wakifunga.

Yanga sasa inarejea kujiandaa na mchezo wake wa kuwania ku­fuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Jumamosi wiki hii dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Waliopata kwa Singida ni Shafiq Batambuze, Tafwadza Kutinyu, Kenny Ally na Elinyesia Sumbi, aliyekosa ni Maliki Antiri.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic