April 2, 2018




Baada ya hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho kumalizika jana mjini Singida, Msemaji wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru ametamba kuwa mshindi.

Hatua hiyo ilimalizika kwa Singida United kuungana na JKT Tanzania, Stand United pamoja na Mtibwa Sugar FC ambazo zilitangulia kufika hatua hiyo.

Kufuatia Singida kuiondoa Yanga, Msemaji wa Mtibwa Sugar ametamba kwa kusema kuwa watapambana kuchukua taji hili ili warejee katika mashindano ya kimataifa.

Kifaru alieleza kwa kuzitaja klabu za Singida na Stand United kuwa ni changa huku akijinadi kuwa lazima watazibomoa kirahisi.

Walima miwa hao wa Mtibwa walifuzu kufika nusu fainali ya Shirikisho baada ya kuwaondoa Azam kwa mikwaju ya penati 9-8 baada ya dakika 90 kumalizika suluhu ya 0-0. 

CHANZO: RADIO ONE

4 COMMENTS:

  1. Nakumbuka kuna timu miaka ya nyuma(siyo Simba wala Yanga)ilishiriki michuano ya kimataifa na baada ya kupokea kipigo kikali hapa nyumbani haikupeleka timu kwenye mchezo wa marudio na CAF iliifungia miaka 3,tangu adhabu hiyo timu hiyo haijawahi kupata nafasi ambayo ingeifanya ianze kuitekeleza adhabu yake,timu hiyo si Mtibwa?Kwako Saleh Ally

    ReplyDelete
    Replies
    1. https://www.pressreader.com/tanzania/dimba/20170524/282565903085164

      Delete
    2. Mwaka 2003 haikushiriki michuano yoyote, lakini mwaka 2004 ikashiriki kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka barani Afrika na kuishia raundi ya kwanza licha ya kushinda raundi ya awali.
      Ilipangiwa kuanza na Chemil Sugar ya Kenya na kuiondoa mashindanoni kwa jumla ya mabao 4-1, ikishinda 2-0 ugenini kabla ya kuibuka na ushindi mwingine wa mabao 2-1 hapa nyumbani.
      Baada ya kutinga hatua ya 32 bora walikutana na Santos ya Afrika Kusini na katika mchezo wa kwanza Mtibwa Sugar walichapwa mabao 3-0 na kugomea kwenda kucheza mechi ya marudiano, hivyo Santos kupewa ushindi mwingine wa pointi 3 na mabao matatu.

      Delete
  2. hakuna tofauti kubwa kati ya mtibwa na singida united na kiukweli mtibwa haina international players kama singida united hivyo kifaru anatakiwa kuwaheshimu. Stand united pamoja na singida united wana makocha wa kimataifa na wazoefu wa mpira wetu kulinganisha na wa azam ambaye bado mgeni.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic