Mshindi mara tano wa tuzo ya Ballon d'Or, Cristiano Ronaldo anataka Manchester United ikishinde mechi yake ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Chelsea, Jumamosi.
Uthibitisho wa hilo ni pale Ronaldo alipoamua kumpa moyo zaidi mshambuliaji kinda wa Man United Murcus Rashford.
Ronaldo amemtumia Rushford jezi yake akiwa amesaini yeye mwenye na maneno ya faraja yanayomhimiza kufanya vizuri zaidi.
Kama jezi hiyo haitoshi, Ronaldo amemtumia Rushford viatu aina ya Nike Air Max 97 via range nyekundu na viatu via mazoezi aina ya CR7.
Ronaldo alipata mafanikio makubwa na Manchester United kabla ya kuondoka mwaka 2008 na kujiunga na Real Madrid.
0 COMMENTS:
Post a Comment