April 2, 2018



Kikosi cha Simba SC kimefanya mazoezi yake ya mwisho leo katika Uwanja wa Sabasaba uliopo mjini Njombe.

Simba itakuwa inakibarua dhidi ya wenyeji wa mji huo, Njombe Mji FC, katika mchezo wa ligi kuu bara utakaopigwa majira ya saa 10 jioni.

Njombe Mji itakuwa inaikaribisha Simba ikiwa na kumbukumbu mbaya za kuondoshwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho na Stand United ya mjini Shinyanga.

Tayari timu zote mbili zimeshakamilisha maandalizi kuelekea mchezo mchezo huo wa kesho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic