Na George Mganga
Simba imejificha Morogoro kujifua kabla ya kukabiliana na Yanga Aprili 29 2018, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kikosi hicho kimerejea mjini humo ikiwa ni siku kadhaa zilizopita kuweka kambi ya muda mfupi wakati ikijiandaa na mechi dhidi ya Lipuli.
Wekundu hao wa Msimbazi watakuwa wanaenda kuvaana na Yanga wakiwa vinara kwenye ligi msimu huu, ambapo mpaka sasa wamefikisha jumla ya alama 59 huku watani zao wakiwa na 47.
Wakati Simba ikiwasili Morogoro, Yanga wao wanacheza na Mbeya City leo kwenye Uwanja wa Sokoine, mjini Mbeya.
0 COMMENTS:
Post a Comment