April 26, 2018




Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi (Kamati ya Saa 72) ya Bodi ya Ligi katika kikao chake kilichopita ilipitia taarifa na matukio mbalimbali na kufanya uamuzi ufuatao;



Mechi namba 185 (Yanga 1 vs Singida United 1). 
Klabu ya Singida United imepigwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kutumia mlango usio rasmi kuingia uwanjani katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 11, 2018 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kitendo hicho ni ukiukaji wa Kanuni ya 14 (14) ya Ligi Kuu kuhusu taratibu za Mchezo, na adhabu dhidi ya klabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 14 (49) ya Ligi Kuu kuhusu Taratibu za Mchezo.

Vilevile Bodi ya Ligi imepeleka malalamiko kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) dhidi ya Meneja wa Singida United, Ibrahim Mohamed kwa kuongoza vurugu za timu yake kulazimisha kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic