April 26, 2018



Na George Mganga

Zikiwa zimesalia siku tatu pekee kuelekea mechi ya Ligi Kuu Bara itakayowakutanisha watani wa jadi, Simba na Yanga, Aprili 29 2018 Jumapili ya wiki hii, yajue machache kuhusiana na DABI hii ambayo huwa na msisimko wa aina yake nchini.

Timu hizi zote zipo mjini Morogoro hivi sasa zikijinoa kwa ajili ya mechi hiyo ya Jumapili itakayofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba wako Uwanja wa Jamhuri huku Yanga wakiwa Uwanja wa Chuo cha Biblia.

Ni nadra timu hizi kuweka kambi ya maandalizi sehemu moja lakini msimu huu zimeamua kufanya maandalizi kwa kuweka kambi mji mmoja. Mara nyingi zimekuwa zikisafiri kuelekea Zanzibar kuweka kambi kati ya Pemba na Unguja.

Simba inaenda kucheza na Yanga ikiwa mbele kwa michezo miwili mbele ya Yanga ambapo imecheza jumla ya mechi 25 huku Yanga ikiwa na 23.

Mbali na michezo, Simba ndiyo vinara wa ligi ambao wamejikusanyia alama 59 huku Yanga wakiwa na 48.

Katika hatua ya mzunguko wa kwanza timu hizi zilienda sare ya 1-1 katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Simba walijipatia bao lao kupitia kwa Shiza Kichuya na baadaye Yanga wakasawazisha kwa Obrey Chirwa.

Ukiachana na matokeo hayo ya mzunguko wa kwanza, wekundu wa Msimbazi Simba walikuwa na Kocha Mcameroon aliyeondoshwa Joseph Omog na Yanga wakiwa na Mzambia George Lwandamina ambaye ametimkia kwao Zambia ikielezwa ni madai ya mshahara.

Vikosi hivi vyote viwili vitaingia dimbani Jumapili vikiwa na makocha wapya, Simba wakiwa na Mfaransa Pierre Lechantre na Yanga wakiwa na Mkongomani Mwinyi Zahera.

Simba inaenda kucheza kucheza na Yanga ikiwa na badiliko la uwepo wa beki Asante Kwasi aliyesajiliwa msimu wa dirisha dogo akitokea Lipuli FC. Kwasi alijiunga na Simba baada ya mzunguko wa kwanza wa ligi kumalizika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic