April 23, 2018



Na George Mganga

Singida United imeungana na Mtibwa Sugar kucheza fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga JKT Tanzania kwa jumla ya mabao 2-1 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Namfua, mjini Singida leo.

Mchezo huo uliokuwa wa hatua ya nusu fainali, ulishuhudiwa nyavu za Singida United zikianza kutikiswa katika dakika ya 38 kupitia Hassan Matelema. Matokeo hayo yalidumu mpaka dakika 45 za kwanza JKT Tanzania ikiwa mbele kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Singida walikuwa wakipambana kusaka bao la kusawazisha na katika dakika ya 58, Tafadzwa Kutinyu aliipatia Singida bao la kusawazisha lililodumu mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yakiwa 1-1.

Baada ya dakika 90 kumalizika, ziliongezwa zingine 30 'Extra Time' ili kupata mshindi, muda huo wa ziada ulileta faida kwa wenyeji Singida kwa kupata bao lingine la pili dakika ya 98 likifungwa na yuleyule Kutinyu.

Matokeo hayo yanaipeleka moja kwa moja Singida United kwenye fainali ambapo itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar June 2 2018 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Stand ilitinga hatua hiyo kwa kuiondosha Stand United kwa mabao 2-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic