April 23, 2018




Uongozi wa Yanga umefafanua kuhusiana na suala la mshambuliaji wake, Obrey Chirwa kuwa ana kadi tatu za njano.

Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh amesema Chirwa ana kadi moja tu ya njano na si tatu.

Saleh amesema watu wamejichanganya kutokana na matamshi ya mtangazaji wa Azam TV wakati akisema kadi ya Chirwa ni ya tatu.

“Alikuwa akimaanisha katika mchezo ule, Chirwa amepewa kadi ya tatu. Yaani kuna kadi nyingine mbili zilikuwa zimetoka katika mechi hiyo, ile ya Chirwa ikawa ya tatu.

“Chirwa ana kadi moja tu na si tatu kama ambavyo umesikia,” alisema.

Suala la Chirwa kuwa na kadi tatu lilizua mkanganyiko mkubwa baada ya vyombo mbalimbali kuripoti ikiwemo blogu hii.

Lakini meneja huyo amesisitiza katika rekodi za Yanga, Chirwa ana kadi hiyo moja ya njano na atakipiga na Simba kama kawa.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic