April 24, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kuwa hauna hofu na mechi ijayo ya ligi kuu dhidi ya watani zao wa jadi, Simba kwakuwa wanaamini mchezo huo utakuwa wa kawaida.

Mkuu wa Kamati ya Mashindano na Usajili katika klabu hiyo, Hussein Nyika, amesema kuwa mechi hiyo itakuwa ya kawaida kama zingine hivyo haiwapi shida.

Kwa mujibu wa Radio One kuptia Spoti Leo, Nyika amewaomba wanachama na mashabiki wa Yanga kuweka nguvu zao kuelekea mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger itakayopigwa Mei 6 huko Algiers.

Kiongozi huyo amefikia hatua ya kuwataka mashabiki wafanye hivyo kwasababu mechi ya Simba haitowapa tabu, na akitamba kuwa wanajiamini.

Yanga imeweka kambi mjini Morogoro ikijiandaa na mechi hiyo ambayo husisimua hisia za watu kabla na baada ya dakika 90, huku Simba nao wakiwa mjini Morogoro.

Mechi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wadau wa soka nchini, itapigwa Aprili 29 2018 kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic