April 24, 2018



Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Mbeya City umetuma barua katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ukilalamikia maamuzi ya Mwamuzi aliyechezesha mchezo wao dhidi ya Yanga kuwa hakuumudu.

Mbeya City wameeleza mapungufu kadhaa ambayo Mwamuzi alishindwa kuyahimili wakati wa mechi hiyo ya ligi kuu iliyopigwa Aprili 22 2018 kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Barua hiyo imeeleza tukio la Juma Mahadhi kufanyiwa faulo ambayo ilizaa bao la kwanza kwa Yanga ikisema kuwa si halali.

Vilevile imeelezea tukio la mchezaji Mshambuliaji wa Yanga, Mzambia, Obrey Chirwa kumtwanga kiwiko mchezaji wa Mbeya City katika mchezo huo.

Tayari uongozi huo umeshawasilisha barua hiyo kunako makao makuu ya TFF yaliyo mitaa ya Karume, Ilala, jijini Dar es Salaam.

3 COMMENTS:

  1. wenzao wamepeleka rufaa wao wamepeleka malalamiko ..............nazi mbovu harabu ya nzima

    ReplyDelete
  2. Kweli kabisa ilitakiwa Chirwa apewe card nyekundu wanabebwa sana hao

    ReplyDelete
  3. ni kawaida yanga kubebwa maana walizoeshwa ushindi kwa kubebwa na malinzi. Goli la Yanga sio sahihi sababu lilipatikana kupitia faulo ambayo haikuwa sahihi. Goli la mbeya city lilikuwa ni goli la video. mbeya city walipiga mpira mwingi sana tena wakiwa pungufu. mbeya city walistahili ushindi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic