Beki kisiki wa Yanga, Kelvin Yondani leo amerejea mazoezi na kuungana na wenzake.
Yondani jana alishindwa kufanya mazoezi na wenzake wakati Yanga ikijifua katika kambi yake mjini Morogoro.
Yanga iko Morogoro kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wake Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.
Yondani amefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Highland mjini Morogoro ikiwa ni maandalizi ya mwishomwisho kabla ya Jumapili.
Muandishi hakuelezea kilichomfanya Yondani kutoshiriki mazoezi ya kwanza na kujiunga jana. Nini lilikuwa tatizo lake?
ReplyDelete