April 18, 2018


Baada ya kuondolewa katika mashindano ya CECAFA, Uongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), kimemcharukia Katibu wa Mkuu wa Baraza hilo, Nicholas Musonye.

Musonye ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati, ametuhumiwa kuifanyia njama za kuiondoa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Karume Boys, baada ya kubainika kuwa wachezaji 12 wamezidi umri.

Kwa mujibu wa Chama hicho, kimeeleza kuwa Musonye amekuwa hana maelewano mazuri na Zanzibar kuhusiana na mashindano hayo, hivyo ametumia kama mbinu ya kuwakomoa kwa kuwaondoa sababu ya kisingizio cha kuzidi umri wa wachezaji, uongozi ulieleza.

Kutokana na tukio hilo kutokea, uongozi wa ZFA umekemea kitendo hicho wakisema kuwa wameonewa ikiwa ni siku moja baada ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kusema itaingilia kati kufanya uchunguzi juu ya kuondolewa kwa kikosi cha Karume Boys.

Mbali na Karume Boys, Ethiopia nayo ilikumbana na rungu la kuondolewa sambamba na faini ya kiasi cha dola za kimarekani 15,000, kutokana na wachezaji kadhaa kuzidi umri stahiki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic