May 14, 2018



Wakati Simba ikijiandaa kuelekea kwenye Ukumbi wa Bunge leo jijini Dodoma kupata pongezi baada ya kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Kocha wa Dodoma FC, Jamhuri Kihwelo 'Julio' jana aliungana na kikosi hicho kupata mlo wa usiku.

Simba ilifanyiwa hafla fupi na Wabunge wanaoishabikia Simba jijini humo baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Dodoma FC uliopigwa jijini humo jana.



Julio aliweza kujumuika na kikosi cha Simba kupata mlo wa usiku huku wakifurahia pamoja kuupata ubingwa huo baada ya kuukosa kwa muda mrefu.

Julio ambaye aliwahi kuwa Kocha Msaidizi wa Simba na sasa Dodoma FC, aliwahi kuomba nafasi ya kuifundisha Yanga baada ya Kocha George Lwandamina kuondoka.

Kikosi hicho kinatarajiwa kuanza safari ya kurejea jijini Dar es Salaam leo ama kesho kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika Uwanja wa Taifa.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic