Na George Mganga
Naibu Waziri wa TAMISEMI nchini, Mh, Joseph Kakunda, amefunguka kuhusiana na kikosi cha Simba kuhusiana na ushiriki wake katika mashindano ya kimataifa akiamini kuwa hakitawapa presha.
Kakunda ameeleza hayo leo Bungeni baada ya kukaribishwa na Mwenyekiti wa kutano wa kikao cha Bunge kujibu moja ya maswali ambayo wizara yake iliulizwa.
Kakunda amesema kuwa anaamini sasa wamepatwa mwakilishi mzuri kwenye michuano ya kimataifa ambapo Simba watashiriki Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
"Sasa ninaamini watanzania tumepata wawakilishi kwenye michuano ya kimataifa ambao hawatatupa presha" amesema Kakunda.
Kauli hiyo imekuja kufuatia Simba kufanikiwa kuutwaa ubingwa wa ligi msimu huu wakiwa wamesaliwa na michezo mitatu mkononi.
Kakunda ametamka kauli hiyo wakati kikosi cha Simba kikiwa ndani ya Bunge baada ya kupata mwaliko maalum na lengo mahususi ni kupokea pongezi za ubingwa wa Ligi Kuu Vodacom kwa msimu wa 2017/18.








pale unaposhindwa kuzuia hisia zako kiprotokali
ReplyDeleteHisia ni ukweli usiopingika jamani
ReplyDeleteHhhhhh, ... @Geofrey Chambua unanvunja mbaav zangu wewe. Ushabiki wa timu ni kitu cha wazi kabisa. Huwa humuoni Mh. Mwigulu Nchemba katika kushabikia Mayebo? Au hilo walikubali, na wengine wakifanya hivyo waona ni uvunjaji wa protokali??
ReplyDelete