May 26, 2018


Na George Mganga

Rasmi uongozi wa Azam FC umethibitisha kuingia mkataba wa mwaka mmoja na aliyekuwa mchezaji wa Yanga, Mzibambwe, Donald Ngoma.

Ngoma amejiunga na Azam baada ya kusitishiwa mkataba wake na Yanga kutokana na kuwa majeruhi wa muda mrefu hivyo kushindwa kugharamika juu ya matibabu yake.

Ngoma alishindwa kukitumikia kikosi cha Yanga kwa takribani msimu mzima wa 2017/18 kutokana na hali yake kiafya kutoruhusu kucheza hivyo kuendelea kuwa nje ya kikosi.

Azam sasa watagharamika kwa ajili ya matibabu ya mchezaji huyo ambaye mpaka sasa ni majeruhi, na taarifa zinaelezwa kuwa watampelekea Afrika Kusini kufanyiwa vipimo vya afya.

Ngoma alijiunga na Yanga akitokea FC Platnum ya Zimbambwe mnamo mwaka 2015 wakati huo Mfanyabiashara, Yusuph Manji akiwa Mwenyekiti wa klabu hiyo.

3 COMMENTS:

  1. Tazama tafauti. Mchezaji kaumia wakati akiichezea Yanga. Yanga ikashindwa kumpstia matibabu na wakasema anawasummbua kwakuwa ana majaraha na wakamtupa nje. Azam imemuokota na jambo la kwanza wao ndio wanaompeleka nje kwa matibanu bila ya shaka kwa mamilioni ya shilingi. Unaona uungwana hu. Ama kweli samaki akichcha usimtupe mtafutie viungo umkaushe. Atamuokota mwenzio ulie na ujute

    ReplyDelete
  2. azam awamefanya kitu ambacho ni sahihi sana! huwezi kusema kuwa mcezaji ni majeruhi halafu ukamuacha tuu bila kuhangaika na suluhisho la hayo majeraha! Mwiba huo unaweza ukawachoma msimu ujao

    ReplyDelete
  3. Ha ha haaaa:::...ni wakati wa MOI kuhama kutoka mitaa ya Twiga na Jangwani kwenda Chamanzi. Wengine nao wanakuja. Anaesema aliachwa anakosea...Yanga ina mkataba wa matibabu na moja ya Hospital kubwa hapo Dar kuhusu matibabu ya wachezaji...unakumbuka ilishawahi kuleta malumbano baina ya Daktari na mgonja. Daktari kasema kapona na anaruhusiwa kuanza mazoezi yeye akasema hajapona. Wakampeleka Afrika Kusini kwenda kuangalia tena..ikaonekana kapona na anaweza kuanza yeye akasema hajapona. Mwisho wa siku akaondoka kwenda Zimbabwe akarudi na cheti feki feki cha daktari wa huko. Mbaya zaidi timu ya Taifa lao ikamtaja kwa ajili ya mechi. Yanga wakaendelea kumvumilia hadi sasa na mshahara wake wamempa wote. Kaondoka akiwa hadai Yanga. Ndio maana hata Kocha Mpya kamwambia "alitakiwa asilipwe kwa kuwa hajafanya kazi yoyote". Julize "unagombana na mkeo na unasikia kuna mtu anamfata...unamuacha na huyo mtu anamchukua...wewe utawaza nini???". Hii ndio taswira ya mpira hapa Bongo...wachezaji wanatupeleka kwa kuwa timu nyingi hazina mfumo wa scouting ..tunasubili nani kaleta na mwingine achukue. Pia viongozi wa timu nyingine kutumia ushawishi feki kwa wachezaji wanaoonekana ni mwiba kwao

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV