May 26, 2018


Nyota inaendelea kumuwakia beki kiraka wa Simba, Shomari Kapombe kwani sasa taarifa zinasema anatakiwa na moja ya timu iliyopanda kucheza Ligi Kuu ya Hispania msimu ujao.

La Liga ni ligi kubwa Ulaya ambapo mas­taa mbalimbali wanacheza wakiwemo Lionel Messi wa Barce­lona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.

Chanzo cha habari kutoka ndani ya Simba, kimeeleza kuwa timu kubwa kutoka His­pania ambayo imepanda ligi kuu inamtaka Kapombe alipokuwa akiichezea Simba mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry ya Misri baada ya kuvutiwa na uwezo wake.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi lilimtafuta Kapombe ili aweke wazi kuhusiana na taarifa hizo, am­bapo alisema: “Nikweli kuna mawakala zaidi ya watatu wamenipigia hivi karibuni wakini­taarifu uwepo wa timu zaidi ya tatu kunihitaji.”

“Wakala wa kwanza ameniambia kuna timu ya Hispania inanitaka, lakini pia zipo zingine mbili, moja kutoka Urusi na nyingine ipo Bara la Asia ambazo zote nimeshataari­fiwa kuni­hitaji, hivyo wakala wangu ameniomba nitume tu baadhi ya ‘clip’ (video) zangu ili aweze kuka­milisha dili hilo.

“Hii ni bahati sana kwangu kuonekana kwa muda mfupi huu ambao nimecheza Simba, japo nia yangu ningependa kuendelea kuwa hapa ili nijiweke vizuri zaidi kwani nina malengo mengi sana ambayo bado sijayafi­kia pamoja na kwamba wao wameshaona uw­ezo wangu,” alisema Kapombe.

6 COMMENTS:

  1. Safi sana kapombe. Siku zote kizuri hujiuza tu wala hakihitaji makelele kukinadi. Kwa tunavyomfahamu kapombe kama atakuwa fiti akikanyaga Spain tu, ukisikia yupo Real Madrid sio jambo la kushangaza ni kijana mwenye nizamu,kujituma na adabu ya kutosha. La Msingi kutoka kwa viongozi wake wa SIMBA wajarbu kumuekwa mazingira rahisi ya kutua Spain kuliko hizo sehemu nyengine.

    ReplyDelete
  2. Dahh huyu jamaa ana bahati sana na Simba,

    ReplyDelete
  3. Wale wa Sunderland walishaenda ? Bongofix

    ReplyDelete
  4. Simba imekuwa daima chimbuko la nyota wanaogombaniwa ughaibuni kuliko timu zote za nyumbani na imekuwa ikiwabariki wachezaji hao kila inapotokea fursa kama jizo kwenda kujipatia riziki zao bila ya kinyongo baadya kuwalea na kuwatakia kila la heri bila ya kinyongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic