May 8, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha klabu ya Yanga kinatarajia kuwasili mchana wa leo jijini Dar es Salaam kikitokea Algeria kwa ajili ya michuano ya Kombe la Shirikish Afrika.

Yanga ilikuwa na kibarua Jumamosi ya wiki hii ikicheza mchezo wa kwanza katika mashindano hayo ukiwa ni wa hatua ya makundi na kukubali kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya U.S.M Alger.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa baada ya kikosi hicho kuwasili kitapumzika leo Jumanne huku Jumatano kikitarajia kusafiri kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

Tanzania Prisons watakuwa wanaikaribisha Yanga Mei 10 2018 Alhamis ya wiki hii kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.




2 COMMENTS:

  1. Wakipigwa au kutoka sare, sisi tunainua kwapa na wake zetu nyumbaniiii. Prison leteni raha hiyo Alhamisi ili tukale alizeti za Singida bila pressure๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚

    ReplyDelete
  2. Je waliogomea safari ya Al Jeria safari hii wataungana na timu yao bila ya kufanya mazoezi yoyote na wenziwao kwa zaidi ya wiki,?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic