May 8, 2018



Baadhi ya mashabiki wa Yanga wameutaka uongozi wa kikosi hicho kufanya maamuzi magumu kuhusiana na kikosi chao ambacho kimekuwa hakina mwenendo mzuri katika msimu huu.

Kauli hiyo imekuja kufuatia Yanga kupoteza mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho katika hatua ya makundi Afrika dhidi ya USM ALger kwa jumla ya mabao 4-0 Jumapili ya wiki iliyopita.

Wapo walioeleza kuwa inabidi Yanga waanze na waliotia mgomo kuisaliti timu ilipoelekea Algeria kwa ajili ya mchezo huo wa juzi Jumapili.

Mashabiki hao baadhi wameeleza Yanga inabidi ikisafishe kikosi upya ikiwemo kuwapunguza wakongwe na kuwa na damu changa ambayo inaweza kutia morali kwenye kikosi ili kiweze kufanya vizuri.

Vilevile wachezaji wote wanaoonekana kuwa ni mizigo ndani ya timu wafanyiwe mpango wa kuondoshwa wakieleza kuwa hawana msaada wowote ndani ya Yanga.

Licha ya kutaka kusafisha kikosi, wapo pia waliokipongeza kikosi hocho licha ya kupoteza huku wakiwapa matumaini wachezaji kuchukulia matokeo hayo kama sehemu ya mchezo wa siku zote katika mpira.


2 COMMENTS:

  1. Tatizo la Yanga ni ukosefu wa fedha kwa ajili ya kuhudumia timu. Kuwalipa wachezaji mishahara kwa wakati pamoja na benchi la ufundi. Inawezekana pesa ipo kiasi ila inatumiwa ndivyo sivyo na viongozi na baadhi ya watu walio karibu na viongozi. Haiwezekani timu ina wadhamini zaidi ya watatu bado mnalia njaa,hao viongozi watakuwa wanahusika na matumizi mabaya ya fedha za klabu au kuna watu wanachukua 10% kwenye fedha za wadhamini zinazotolewa kwaajili ya klabu. Hii timu ina hitaji viongozi wenye uzalendo wa kweli kuipigania klabu. Wanashindwa kuondoa bechi la ufundi kwasababu hawana fedha za kuwalipa kuvunja mikataba yao, wanashindwa kumpa mkataba kocha mpya kwasababu hawana fedha ya kumlipa, wanashindwa kumwacha ngoma na tambwe kwakuwa hawana fedha za kulipa kuvunja mikataba yao. Wameshindwa kujikubali na kuishi kulingana na uwezo wao bado wanalazimisha kuishi katika daraja la juu kama enzi za Yusuph Manji na ili kufanya hivyo wanaishi kwa kukopa kopa na ulaghai wa mjini mjini. Mficha maradhi kifo umuumbua. Hawashauriki viongozi hawa ama la wanaziba masikio ili waendelee kujineemesha kwa fedha za Yanga. Ipo siku tutawaona wanapanda magari ya magereza kwenda mahakamani. Kila jambo lina mwisho wake na uongo una mwisho wake, mwisho wa uongo ni ukweli, mwisho wa giza ni mwanga, mwisho wa usiku ni asubuhi mapambazuko. Uongozi wa Yanga utambue utapeli huu una mwisho wake na ni mwisho mchungu kwao. Waitishe mkutano mkuu mapema na wajiuzulu na waseme pesa za sportpesa, azam tv, vodacom, macron, maji ya uhai, caf zipo wapi na zimetumikaje. Kwanini wachezaji wanalia njaa.!!!

    ReplyDelete
  2. Hata mkifukuza wachezaji na kuleta wapya, hao wapya hawatakuwa tayyari kufanya kazi bila ya malipo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic