Manchester United wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred, 25, na wana matumaini ya kukumilisha shughuli hiyo ifikapo wiki ijayo. (Manchester Evening News)
United wameanza mazungumzo na Tottenham ya kumsaini mlinzi Toby Alderweireld, 29, lakini Tottenham wanataka pauni milioni 75 kwa mbelgiji huyo. (Mirror)
Mchezaji anayewindwa na Manchester City Jorginho, 26, atafanya mazungumzo na Napoli wiki ijayo huku Mbrazil huyo anayewekewa thamania ya pauni milioni 52 akiwa na nia ya kuhamia klabu ya Premier League. (Sun)
Manchester City watahitaji kulipa pauni milioni 60 kumsaini wing'a wa Leicester Riyad Mahrez, 27, ambaye walijaribu kumsaini mwezi Januarai. (Guardian)
Meneja wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri, ambaye mabala pake palichukuliwa na Carlo Ancelotti, hajaafikia makubabaliano na Zenit St Petersburg wakati anataka kujiunga na Chelesea. (Mail)
Kiungo wa zamani wa kati wa Chelsea Michael Ballack anaweza kurudi Stamford Bridge kuwa mkurugenzi mpya wa kandanda wa klabu hiyo. (Evening Standard)
Tottenham wamejiunga kwenye mbio za kumsaini beki wa West Brom raia wa Misri Ahmed Hegazi, 27. (ESPN)
Atletico Madrid na Inter Milan wote wanataka kumsaini mshambuliaji wa West Brom Salomon Rondon, 28, na raia huyo wa Venezuela anapatikana kwa pauni milioni 16 baada ya klabu hiyi kuondolewa kutoka Premier League. (Sky Sports)
Atletico wamempa ofa mshambuliaji wao wa umri wa miaka 27 Antoine Griezmann pauni milioni 8.75 zaidi ya Barcelona ili Mfaransa huyo apate kubaki katika klabu hiyo. (Mail)
Meneja mpya wa West Ham Manuel Pellegrini anataka kumfanya kipa wa Reims Edouard Mendy, 26, kuwa mchezaji wa kwanza ambaye atamsaini. (Mirror)
Real Betis wamejiunga na wenzao katika ligi ya La Liga, Athletic Bilbao kumwinda kiungo wa kati wa Newcastle Mikel Merino, 21. (AS - in Spanish)
Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anatathmini kumwinda mchezaji wa Ajax raia wa Uholanzi Matthijs de Ligt,18. (Guardian)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anafikiria kuchukua likizo kutoka kandanda ikiwa atafutwa na klabu hiyo. (Telegraph)
Kutoka BBC
0 COMMENTS:
Post a Comment