May 16, 2018


Baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kupitia Rais wake, Wallace Karia, kutuma maombi Wiazara ya Michezo likiomba ugeni rasmi kutoka kwa Rais wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuwa mgeni rasmi mechi ya Simba dhidi ya Kagera, Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga nchini, Bakili Makele afunguka.

Makele ameeleza kuwa yeye kama Mwenyekiti wa Matawi ya Yanga nchini pamoja na Yanga kwa ujumla hawana kinyongo na suala hilo kutokana na ombi hilo la TFF kumuhitaji Rais Magufuli awe mgeni rasmi.

Mwenyekiti huyo amesema kuwa kumekuwa na baadhi ya maneno ambayo yamekuwa yakielezwa kuwa Yanga imepatwa na kinyongo sababu bingwa wa nchi amekuwa Simba, jambo ambalo amesema si sahihi.

Makele amefunguka kwa kueleza Simba ndiye bingwa wa nchi kwa sasa na wanastahili pongezi kutokana na kazi kubwa waliyoifanya msimu huu.

Aidha, Makele ameipongeza serikali na Rais Magufuli endapo atahudhuria katika mchezo wa Simba na Kagera ambao utakuwa na hafla ya kuwakabidhi Simba taji la ligi Mei 19 2018 kwenye Uwanja wa Taifa.

Mbali na Simba, Magufuli atawakabidhiwa Kombe la CECAFA (U17) walilolitwaaSerengeti Boys huko Burundi kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali.

10 COMMENTS:

  1. Maneno kuntu hayo, hongera mwenyekiti

    ReplyDelete
  2. Maneno kuntu hayo, hongera mwenyekiti

    ReplyDelete
  3. Hayi ndiyo maneno ya MTU aliyekomaa kimichezo. Hongera mwenyekiti, umedhihirisha ukomavu wa kimichezo. Hiyo ndio inaitwa FAIR PLAY!

    ReplyDelete
    Replies
    1. angekuwa Manara sasa hapo........

      Delete
  4. Wafa maji tu cimbwa kila kitu hawajiamin mpk waitaje yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndugu yangu siyo kosa la Simba, bali ni Purizonz ya Mbea ndio waliwadhuru kandambili. mtausikia ubingwa kwenye bomba tu, tofauti ya point ishruun. Mmezoea ubingwa wa magoli ya mikono ya tambwa, na ya rufaa za kagela shuga. mtabaki kujiliwaza na historia tu, eti miaka mitatu, mitano etc. SImba ndiyo Bingwaa. This is Simba brother!

      Delete
  5. Kuna comments zimenifurahisha sana hapo Juu,Ila ingekuwa wao wangeongea shombo balaa,Ila wekeni akiba ya maneno ikitokea upande wa pili nao wakichukua ubingwa na wakakabidhiwa na rais mpongeze pia

    ReplyDelete
  6. Mimi sioni shida kwa mawazo ya mtu kupinga. Ila uongozi ndo umeamua siyo klabu ndo imeomba wakabidhiwe kombe na Rais, shida ni nini ndugu? Upande wa pili umefanya nini tena?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Upande wa pili walishaanza kutoa poov jana. Kwamba eti ni kuchanganya michezo na siasa. Wakati JK anachekelea ushindi wao wa kuhonga tiefuefu wao walikuwa wakijisikia high! Wenzao wametoka jasho kushinda kombe, wao hawataki na wananuna

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic