BEKI ARSENAL AISABABISHIA MAJANGA TIMU YA TAIFA YA UFARANSA, NJE YA DIMBA KWA MIEZI SITA
Beki wa klabu ya Arsenal, Laurent Koscielny, atakosekana nje ya dimba kwa muda wa miezi 6 baada ya kuumia mguu.
Koscielny aliumia mguu wake katika mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya nusu fainali katika UEFA Europa League dhidi ya Atletico de Madrid uliopigwa nchini Spain Alhamis ya wiki iliyopita.
Bei huyo ameumia zikiwa zimesalia wiki kadhaa tu kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza huko Russia.
Kwa mujibu wa Kocha wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amesema kuwa mchezaji huyo atakosa rasmi michuano ya Kombe la Dunia inayotaraji kuanza mwezi ujao huko Russia.








0 COMMENTS:
Post a Comment