May 8, 2018



Kikosi cha Yanga kimewasili salama jijini Dar es Salaam kikitokea Algeria kushiriki mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger.

Yanga imerejea nchini baada ya kupoteza mchezo huo wa hatua ya kwanza katika makundi kwa jumla ya mabao 4-0.

Baada ya kuwasili Dar es Salaam leo, Yanga itaondoka kuelekea Mbeya kesho kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Tanzania Prisons itakuwa inawakaribisha Yanga jijini Mbeya ambapo mchezo huo utapigwa kwenye Uwanja wa Sokoine Alhamis ya keshokutwa kuanzia majira ya saa 10 jioni.

1 COMMENTS:

  1. Tuwekee picha za mapokezi tuone mimba fc waliporejea.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic