Kama unawadharau basi unajidanganya, maana Yanga wako fiti hasa.
Wao wenyewe wamesema wako tayari kwa ajili ya mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika, hatua ya makundi dhidi ya mabingwa wa Rwanda, Rayon Sports ya Rwanda, kesho.
Mchezo huo unatarajiwa kupigwa kesho saa moja kamili usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambao Yanga wanahitaji ushindi ili wajiwekee mazingira mazuri ya kuvuka hatua ya robo fainali.
Yanga inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa mabao 4-0 na Waarabu wa Algeria, kikosi cha USM Alger.
Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Noel Mwandila alisema katika mechi hiyo wataingia uwanjani kwa lengo moja pekee la kuchukua pointi tatu muhinu pekee.
Mwandila alisema, anafurahia kurejea wachezaji wao waliopona majeraha Obrey Chirwa, Amissi Tambwe na Thabani Kamusoko ambao anaamini uwepo wao kutaimarisha kikosi chao.
"Ili tuweze kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hii, basi ni lazima tuwafunge Rayon katika mechi hii ya nyumbani kabla ya kwenda kurudiana kwao," alisema Mwandila.
Hata hivyo, Yanga itawakosa baadhi ya wachezaji akiwemo Said Makapu mwenye adhabu ya kadi, Papy Tshishimbi majeruhi aliyeelezwa kurejea kwao DR Congo kwa matibabu zaidi na Ibrahim Ajibu.







Tupo tayari uzalendo kwanza msituangushe
ReplyDelete