May 15, 2018


Baada ya kuitandika Stand United kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi, Msemaji wa timu hiyo Masau Bwire, amewatumia salaam Yanga.

Bwire amewatambia Yanga akieleza kuwa ni zamu yao sasa kupapaswa baada ya Stand kukubali bao hilo moja.

Ruvu baada ya mechi na Stand itakuwa inajiandaa kucheza na Yanga inayotarajia kushuka dimbani kesho Uwanja wa Taifa kukipiga na Rayon Sports ya Rwanda.

Yanga itakuwa inacheza mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ule wa kwanza kwenye hatua hiyo ya makundi kupoteza kwa mabao 4-0 dhidi ya USM Alger.

1 COMMENTS:

  1. Watapiga za ulaya ulaya,mwendo wa kupapasa tu,jamaa anaongea sana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic