Mahakama ya Hispania imemhukumu mshambuliaji nyota wa Monaco, Radamel Falcao kwenda jela miezi 16 na faini ya euro million tisa.
Mahakama hiyo imempata aria huyo wa Colombia na hatia ya kukwepa kodi kwa miaka miwili mfululizo.
Falcao aaliyewahi kukipiga Manchester United na Chelsea za England anaonekana alikwepa kodi nchini Hispania wakati akiichezea Atletico Madrid.
Hata hivyo, Falcao ana nafasi ya kukwepa kifungo hicho kwa mujibu wa sheria za Hispania kama ataweza kulipa kwa makubaliani anachodaiwa.
Imeelezwa na mahakama hiyo kwamba alikwenda kodi hivi;
mwaka 2012 alikwepa kodi kwa kiasi cha euro 822,609 euros, halafu akarudia mwaka 2013 kwa kukwepa kulipa kitita cha euro 4,839,253.
Wachezaji nyota wanaocheza nchini Hispania, wakiwemo Cristiano Ronaldo na Lionel Messi wamewahi kuingia kwenye mgogoro huo wa masuala ya kodi.
Lakini wako ambao waliingia katika msukosuko huo hadi kuhukumiwa kama Xabi Alonso, Angel Di Maria, Ricardo Carvalho, Luka Modric na Marcelo.
0 COMMENTS:
Post a Comment