May 23, 2018



Zile taarifa kwamba mkongwe Andres Iniesta atacheza soka nchini Japan, zimeanza kutimia.

Hii ni badaa ya Iniesta ambaye amestaafu kuichezea FC Barcelona kusafiri hadi nchini Japan kwa ndege maalum ya kukodi kumalizia mazungumzo ya mwisho.

Taarifa zinaeleza, Iniesta atajiunga na Vissel Kobe ya nchini Japan na ametupia picha mtandaoni akiwa na boss wa klabu hiyo, Hiroshi Mikitani, na sasa inaonyesha hakuna ubishi kwamba atacheza katika ligi ya nchini hiyo maarufu kama J1 League.

Tayari inaonekana kuna mvuto wa uhusiano kwa kuwa FC Barcelona inadhaminiwa na kampuni ya Raukaten ambayo ndiyo mdhamini mkuu pia wa Vissel Kobe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic