HAJI MANARA APINGA KUONDOKA SIMBA, BADO NI MNYAMA HALISI
Na George Mganga
Baada ya kuenea kwa taarifa zilizoeleza kuwa Ofisa wa Habari katika klabu ya Simba. Haji Manara, kuwa anataka kuachia ngazi, Manara ameibuka na kukanusha.
Manara ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram hivi punde akisema hawawezi akaondoka Simba wakati mgumu kama huu huku akiwataka Wanasimba kilichotangazwa ni uzushi.
Awali baadhi ya mitandao na vyombo kadhaa vya habari vieleza kuwa yawezekana Manara akawa anataka kuachia ngazi kufuatia kauli ya mafumbo aliyoaiandika jana katika ukurasa wake wa Instagram ambayo ilishindwa kutafsrika kirahisi.
Kushindwa kueleweka kwa kauli hiyo kirahisi, kiliwafanya baadhi ya wadau wa soka na vyombo kadhaa vya habari kuripoti kuwa pengine Manara anaashiria kuachana na vinara hao wa ligi msimu huu.
"Siondoki Simba na naomba muelewe hvyo, ninafanya kazi sehemu sahihi na wakati sahihi. Rafiki zangu na washabiki wa klabu muelewe hvyo. Walichokitangaza ni uzushi, nawezaje kuwaacha Simba kipindi hiki muhimu?" ameandika Manara.








Vipi utaitaja Simba bila ya kumtaja Manara na vipi utamtaja Manara bila ya kuitaja Simba. Huyo mtoto wa Simba mpendwa.
ReplyDeleteLoo, yanga walikuwa wameshafurahi, waafikiri kama vile Manara ndio MO Dewji. Eti simba kwisha
ReplyDelete