Hatua hiyo imefikia kutokana na timu hiyo kuwa katika mazingira hatarishi ya kuteremka daraja kutokana na maendeleo ya msimu huu kuwa mabaya.
Maendeleo ya Ndanda kwa msimu huu yamewafanya mashabiki wa timu hiyo kuwaomba wachezaji kusahau matatizo yote ikiwemo fedha wanazodai kabla ya kuwakabili Simba mwishoni mwa wiki hii kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ndanda imekuwa haina matokeo mazuri ambapo mpaka sasa imekamata nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 huku ikicheza jumla ya michezo 26.
Simba itakuwa inawakaribisha Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya ligi itakayoanza majira ya saa 10 kamili jioni.








Watu wana njaa. Vipi tumbo tupu laweza kuchemka wataweza wapi kutaharaki mbele ya nyama hatari Simba? Haiingii akilini
ReplyDelete