May 8, 2018



Na George Mganga

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano katika klabu ya Simba, Haji Manara, ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha kikao maalum kwa ajili ya kujadili suala la Yanga kupoteza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ilikuwa ina kibarua cha mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho katika hatua ya makundi dhidi ya USM Alger uliopigwa Jumapili iliyopita mjini Algiers, Algeria na wanyeji kuibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Manara ameliomba Bunge kuitisha kikao maalum kujadili namna Yanga ilivyofanya vibaya akieleza kuwa inawezekana suluhisho la tatizo hilo linaweza kupatikana.

Mbali na kuomba kikao kuitishwa bungeni kuijadili Yanga, Manara amesema amepokea matokeo hayo kwa masikitiko makubwa kutokana na kipigo ambacho watani zake wa jadi wamekipata huko Algeria.

"Ni matokeo mabaya, kusema tu ule ukweli yamenisikitisha hivyo ni vema wakajipanga kwa ajili ya michezo mingine inayofuata" alisema.

Kikosi cha Yanga kipo njiani hivi sasa kurejea nchini ambapo kinatarajiwa kuwasili majira ya kuanzia saa 6 mchana wa leo.

8 COMMENTS:

  1. hivi na nyie amna habari za maana hadi muandike habari kama hizi badilikeni acheni upuuzi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunapozungumzia matokeo ya yanga timu ya wananchi ina maana tunatambua umuhimu wa bendera manara yupo sahihi sana

      Delete
  2. Wacha hasira. Mlipokuwa mnaitania SIMBA ilikuwa sawa sasa na nyinyi mkitaniwa wacha hasira vumililia.Ndio utani wenyewe.

    ReplyDelete
  3. Bora wangepelekwa ndondo cup timu Ile ya keko

    ReplyDelete
  4. Wameaibisha haina letu

    ReplyDelete
  5. Daah!!!! Mtani kumbe kipigo kinauma eeeheeh!!!! Ila bao nne inabidi zijadiliwe Bungeni, mbona kombe huwa mnaomba kulipeleka bungeni na kupigwa picha na waheshimiwa sasa kwa nini kipigo kisijadiliwe? Nitaomba mwongozo kwa Spika.

    ReplyDelete
  6. Yanga ilikwisha panga kuwa watakusanya mamilioni kila wanaposhinda na waliahidi kukusanya hela nyingi sana wataweza kulipa madeni yao na pia eti kuwanyanganya Simba Kichuya na wengine kutoka Mbeya City. Utafikiri wapo usingizini mnono wakitokwa na polojo na pia hawajakata tamaa ya ubingwa HA.HA HAAA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic