May 8, 2018


Baada ya kuanza vibaya katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Katibu Mkuu wa zamani wa Yanga, Jonas Tiboroha, amesema alipokiona kikosi kilichopangwa kwa ajili ya mchezo alienda kulala.

Tiboroha ambaye aliondoka Yanga na mikoba yake kuchukuliwa na Boniface Mkwasa, ameeleza kikosi hicho kilimfanya akalale mapema na alitarajia kuona yaliyotokea huko Algeria.

Kiongozi huyo wa zamani amesema kikosi hakikuwa kinaleta matumaini zaidi ya masikitiko kwani hakikuwa imara na badala yake kilikuwa na udhaifu mwingi.

Yanga imeshindwa kuanza vema baada ya kupoteza kwa jumla ya mabao 4-0 Jumapili ya wiki iliyopita, mechi ikipigwa Uwanja wa Julai 5 1962 huko Algiers, Algeria.

Kikosi hicho kinatarajia kuwasili leo majira ya mchana kikitokea Algeria kisha kesho kitaanza safari ya kuelekea Mbeya kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons.

1 COMMENTS:

  1. Ni kweli,sio kiongozi Huyo msaafu tu aliyeumizwa na kikosi hicho,Ni kikosi kanakwambwa kimepangwa kucheza ndondo cup sodo v/s Ihemi rangers ya iringa vijijini.
    Siamini macho yangu.inabidi kuwa na uongozi sugu kwenye ujasiri wa ukwapuaji na ufisadi tu kupeleka timu dhaifu kama ile kwa lengo LA kimashindano.Ni viongozi dhaifu pekee wanaoweza kuwatumia wachezaji kama makarai ya kujenga matumbo yao tu.Ni aibu Ni fedheha kwa club,nchi na wanayanga waaminifu.
    Mkwasa na uongozi wake anaua club.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic