Mhariri Mtendaji wa Global Publishers na gazeti la Championi, Saleh Ally, ametoa maoni yake kiufupi kuhusiana na kipa Ramadhan Kabwili kuondolewa katika kikosi cha Ngorongoro Heroes na Kocha Mkuu, Ammy Ninje.
Ally ameungana na baadhi waliopinga suala hilo akisema ni kweli Ninje ameteleza kutokana na kuachwa kwa kipa huyo aliyekuwa tegemeo kwenye kikosi hicho.
Mhariri huyo anaamini bado Kabwili alistahili kupewa nafasi ya kuendelea kusalia langoni kuitumikia Ngorongoro wakati ikielekea kucheza mchezo wa kimataifa wa kufuzu kuelekea AFCON (U20) dhidi ya Mali, Jumapili ya wiki hii.
Upande mwingine Ally amesema Ninje anaweza kuwa sahihi endapo mbadala wake aliyempata anaweza kuwa sawasawa kutuonesha kile alichokuwa anacho Kabwili.
"Pengine anaweza akawa sahihi kama mbadala wake aliyempata anaweza kuwa sawa na Kabwili au zaidi, inaweza kuwa jambo zuri zaidi" amesema Ally.
"Ila kama atakayempanga ataonyesha kiwango cha chini zaidi, basi atakuwa na deni na jambo la kujibu mbele ya Watanzania.
"Pamoja na yote, naendelea kuweka msisitizo kwamba Kabwili ni sehemu ya hazina ya Tanzania, tunajua amepitia wapi katika makuzi ya kisoka.
"Amecheza hadi michuano mikubwa ya Afrika akiwa na timu ya vijana, amecheza Ligi ya Mabingwa akiwa na Yanga, anastahili kabisa kupata nafasi ili tumuendeleze baada ya kumuacha na mwisho tuanze kulalamika kuhusiana na vipaji vinavyoishia njiani."
Hilo gazeti liitwalo global publishers linatoka siku gani,litakuwa ni gazeti jipya hilo maana sijawahi kulisoma
ReplyDeleteUsishangae sana,hii ni blog inayoongoza kwa makosa ya kiuandishi,wenzake tumeshaizoea.
DeleteMakocha wapo wangapi Nchi hii?Kila mtu kocha. Kabwili kachagua Yanga kocha afanye nini?
ReplyDeleteKocha ndiye anayejua
ReplyDelete