May 8, 2018


Shirikisho la Soka nchini TFF limeziagiza klabu za Yanga na Coastal Union kufanya uchaguzi ili kuziba nafasi za viongozi wao walioachia ngazi.

Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF kwenda kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho hilo, Rvocatus Kuuli, imeeleza kuzitaka timu hizo kufanya uchaguzi huo ili kujana nafasi ambazo zipo wazi.

Hivi karibuni aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji aliachia ngazi kuendelea kuitumikia klabu hiyo kwa madai ya kuwa alihitaji kupumzika.

Mbali na Yanga pamoja na Coastal Union, AFC Arusha nayo inatakiwa kuungana na timu hizo tajwa hapo juu kufanya uchaguzi huo.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic