May 5, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga umeeleza kuwa wachezaji wao waliosalia nchini baada ya kukosekana katika msafara wa kikosi kilichosafiri kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho kuwa wana matatizo binafsi na si madai ya mishahara.

Inaelezwa kuwa uongozi huo umesema wachezaji hao wameshindwa kutokana na kukabiliwa na changamoto, ambapo imeelezwa Papy Kabamba na Kelvin Yondani waliumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Simba.

Mbali na wachezaji hao kuwa majeruhi, Mzambia Obrey Chirwa naye amesalia kutokana na kusumbuliwa na ugonjwa wa Malaria hivyo naye amesalia Dar es Salaam ili kuuguza hali yake.

Kumekuwa na taarifa zinazodai kuwa wachezaji hao wameshindwa kusafiri kuelekea Algeri kutokana na mgomo baridi juu ya madai ya stahiki zao ikiwemo mishahara.

Yanga itakuwa inacheza na USM Alger katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shrikisho Afrika, kesho Jumapili kuanzia majira ya saa 4 kamili usiku.

3 COMMENTS:

  1. Kwa sisi tunaoielewa na kuikumbuka vizuri Yanga,Haijawahi kutokea uongozi wenye migogoro na bench I LA ufundi,au wachezaji hapo clubuni kama uongozi huu was B.Mkwasa.shida tupu na kwa hakika hizi in dalili za viongozi wapiga dili,maslaho binafsi na wanakula hadi mbegu.Ni watu wa kutupiwa.macho,uongozi juu ya mwenendo was vlubu in mwingi,maneno ya bandia juu ya mwenendo was wachezaji in mengi.No dalili kuwa club itawafia mikononi mwao.
    Hivi peza zote zinaxoingizwa ktk kila mchezo hazimalizi matakwa ya wachezaji?In mifumo binafsi inaendesha yanga kwa sasa.

    ReplyDelete
  2. Chungu kinachemka iposiku viongozi watasema ukweli wa mambo dunia yaleo siya kuficha ukweli .

    ReplyDelete
  3. Dah haya majanga na hapo Yusuf Manji anaidai klabu shs billioni 11...Jengo na uwanja unadaiwa na Ardhi...wachezaji wanadai malimbikizo ya mishahara.
    Hakuna jinsi zaidi ya kubadilisha mifumo ya uendashaji wa lkabu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic