May 5, 2018



Mshambuliaji wa klabu ya Yanga ambaye ameshindwa kusafiri na timu kuelekea Algeria, Ibrahim Ajibu, inaelezwa amesalia Dar es Salaam kumuangalia mke wake.

Taarifa za ndani kutoka Yanga zinaeleza kuwa Ajibu ameshindwa kusafiri na timu ili kumuangalia mke wake ambaye siku zake zake za kujifungua zimekaribia.

Ajibu ameungana na miongini mwa wachezaji wanzake ambao hawajasafiri ikiwemo Kelvin Yondani, Obrey Chirwa pamoja na Papy Kabamba Tshishimbi waliosalia kutokana na matatizo mbalimbali.

Yanga inashuka dimbani kesho kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho dhidi ya USM Alger utakaopigwa kesho Jumapili.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic