May 9, 2018


Na George Mganga

Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wa Matawi nchini, Bakili Makele, umelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) uwalipe fedha zao haraka wanazozidai.

Kiongozi huyo ameeleza kuwa TFF iliwakata Yanga kiasi cha pesa ambazo ni zaidi ya milioni 200 kupitia VAT baada ya kuingiza mashabiki bure katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe.

Yanga iliingiza mashabiki bure wakati huo ikiwa chini ya Mwenyekiti wake, Yusuph Manji, ambaye alilipia gharama zote za tiketi Juni 18 2016 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Makele ameutupia lawama uongozi wa TFF akisema kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa ilihali wanajua klabu inapitia wakati mgumu hivi sasa haswa katika suala la kuyumba kiuchumi.

Ameongeza kwa kusema kuwa wao wanatakiwa wailee Yanga kama baba wa soka la nchi hii kuliko kuzidi kuikata fedha na kuzidi kuikandamiza.

Aidha, Makele amesema TFF wamekuwa wakifanya utamaduni huo kuzidi kuifanyia dhuluma timu hiyo na pia akieleza hata fedha za mdhamini wa Ligi Kuu Bara, Vodacom kuwa wamebaniwa kupewa.

Mbali na fedha za mdhamini, Makele amefunguka pia kuhusiana na kutopokea vifaa vya CAF kwa ajili ya mashindano ya kimataifa kwa kuilaumu TFF kuwa inahusika kwa maana vinapitia kwao.

Kiongozi huyo wa matawi amewaomba TFF chini ya Rais Wallace Karia, wabadilike na warejee katika usahihi wa ujabikaji ili walitendee haki soka la Tanzania wakiwa kama mlezi mkuu.


6 COMMENTS:

  1. Ukisikia "viporo", hiki ni kiporo og.Leo mnaanza kukumbuka hadi mechi mlizokataa kutoza viingilio?

    Waswahili walisema" mtoto wa kambo hadeki",mlijisahau mkadhani Manji ni baba yenu kumbe ni baba wa kambo,leo kawakimbia sasa mnaanza kukumbuka ofa zake.

    Bado kitambo kidogo mtaanza kudai fedha zilizotumika kuweka kambi Uturuki!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nini za Uturuki hata walikoweka kambi Pemba watadai ...daah siamini kama ndio hawa mashabiki wa Yanga walivokuwa na kejeli na matusi utafikiri walikuwa na share na Manji...pesa walichukua kina Malinzi leo msala wanasema kina Karia. ..usitukane mamba wakati hujavuka mto na kabla hujafa hujaumbwa....Hili ni fundisho tulilopata Simba

      Delete
  2. Aendelee tu kucharuka

    ReplyDelete
  3. Kweli kila ulipo fanya zinaa lazima upakumbue hata ipite dahari na dahari

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nimekipenda sana kiswahili chako hahahaaa!! Wapitiage na huku angalau wajifunze lugha kama si ujumbe unaoandikwa.

      Delete
  4. Heee wa kimataifa kulikoni?....

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic