May 8, 2018



Na George Mganga

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini katika klabu ya Yanga ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), George Huruma Mkuchika, amewataka Wanayanga kutuliza munkari.

Mkuchika amefikia hatua ya kunena hayo kufuatia kikosi cha Yanga kuanza vibaya kwenye mechi ya kwanza ya hatua ya makundi katika Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger kutoka Algeria.

Yanga ilikubali kichapo cha mabao 4-0 ugenini Algiers na kupelekea mashabiki wengi wa Yanga kupandwa na hasira huku baadhi wakikata tamaa juu ya kikosi chao namna kilivyo kwa sasa.

Akizungumza na Radio EFM kwenye kipindi cha Michezo, Mkuchika amewaomba wanachama na mashabiki wa Yanga kuwa watulivu huku akiwaahidi timu hiyo kufanya vizuri kwani mapambano bado yanaendelea.

Waziri huyo ameelza kuwa kwenye mpira kuna aina ya matokeo matatu ambayo ni kufungwa, kufunga na kwenda sare ama suluhu hivyo si vema wakakata tamaa mapema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic