KOCHA AELEZA MIPANGO NA MIKAKATI ILIYOPO SERENGETI BOYS BAADA YA KUTWAA UBINGWA CECAFA
Baada ya kuwasili nchini kikitokea nchini Burundi kikiwa kimefanikiwa kuutwaa ubingwa wa michuano ya CECAFA (U17), Kocha Mkuu wa kikosi cha Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 17 'Serengeti Boys' Oscar Mirambo, ameeleza mipango mipango na mikakati waliyonayo hivi sasa.
Serengeti imefanikiwa kuibuka kidedea katika mashindano hayo kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Somalia kwenye mchezo wa fainali iliyopigwa nchini Burundi.
Mirambo amesema kuwa hivi sasa mipango yao ni kuzidi kukiweka kikosi hicho katika mazingira mazuri ili kiendelee kuwepo na baadaye kiwe nguzo nzuri ya taifa.
Mbali na hilo, Mirambo ameahidi kufanya kazi usiku na mchana akishirikiana na viongozi wenzake ili kukiimarisha na kufikia mwaka 2019 kiwe kipana na kije kufanya vizuri kwenye mashindano ya AFCON kwa baadaye.
Kikosi hicho kimewasili nchini usiku wa kuamkia jana na kupokelewa na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harisson Mwakyembe, sambamba na Rais wa TFF, Wallace Karia.








0 COMMENTS:
Post a Comment