May 7, 2018



Aliyewahi kuwa Kocha wa klabu ya Yanga, Jack Chamangwana, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 61.

Taarifa zinaeleza kuwa Chamangwana amefariki jana jioni katika hospitali ya Malikia Elizabeth iliyopo nchini Malawi baada ya kuumwa kwa muda mrefu.

Taarifa kutoka katika vyombo vya habari vya Malawi, vinaeleza Chamangwana alikuwa katika wakati wa kuumwa na kurejea katika hali yake kabla ya kulazwa kwa kipindi kirefu, hadi mauti yalipomkuta.

Kocha huyo Mmalawi, aliwa kuinoa Yanga na kuiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi mwanzoni mwa miaka ya 2000 kabla ya kurejea kwao Malawi.

Akiwa Malawi aliendelea na nafasi ya ukocha na akateuliwa kuwa mmoja wa wasaidizi wa Kinnah Phiri katika timu ya taifa ya Malawi.

Baadaye alirejea tena kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Malawi 'The Flames', bosi wake akiwa Young Chimodzi na mwaka 1995, wote wawili walitimuliwa kutokana na matokeo mabaya.

Chamangwana aliyekuwa maarufu kwa jina la Afrika aliwahi kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini, pia aliichezea timu ya taifa ya Malawi mechi 133.



Salehjembe.blogspot.com inatoa pole kwa walengwa wote walioguswa na msiba huu mzito. Pumzika kwa amani Chamangwana.


1 COMMENTS:

  1. Umri wa miaka 31? Ebu tuache masihala, uso wake tu unaonesha yeye ni mtu mzima kabisa. Mwandishi embu tafuta umri wake sahihi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic