May 7, 2018



Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano na Usajili, Hussein Nyika, umesema kuwa utafanya mamuzi magumu kuhusiana na mchezaji wake, Donald Ngoma.

Akizungumza asubuhi na Radio EFM asubuhi hii, Nyika, ameeleza kuwa uongozi utakaa na kujlijadili suala la Ngoma na baadaye utaweza kuja na maamuzi ambayo watayatangaza.

Ngoma amekosekana kwa muda mrefu Uwanjani kutokana na kusumbuliwa na majeraha tangu msimu wa ligi uliopita.

Mbali na maamuzi hayo kwa Ngoma, Yanga wamesema watafanya mabadiliko makubwa katika kikosi chao kwa ujumla kutokana na namna kiwango cha timu kilivyo kwa ujumla.

Kauli hizo zimekuja kufuatia kipigo cha mabao manne kwa sifuri dhidi ya USM Alger kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika usiku wa jana.

6 COMMENTS:

  1. Nadhani kwa nia njema Club imalizane naye vizuri, maana hatakama atapona kabisa hawezi kurudi katika kiwango alichokua nacho miaka 2 iliyopita,hivyo ni vema kumalizana naye kwa wema na amani.

    ReplyDelete
  2. Kila siku mnamwekea vikao visivyo na maamuzi ya mwisho kiukweli tu mkataba wa ngoma hamuwezi kuuvunja

    ReplyDelete
  3. Kwani huyu Ngoma si kapata majeraha wakati akiitumikia yanga baada mafanikio makubwa aliuoipa timu na jee baada ya majeraha hayo yanga imefanya nini kuonesha kuwa mnamthamini na sasa shukurani yenu juu yake ni kumsimanga na kumfukuza. Fadhili ya punda ni mashuzi.

    ReplyDelete
  4. Wa kale wamesems, samaki skioza usimtupe, umtafutie viungo umkaushe, atakuja kumuokota mwenzio ulie uje kujuta

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic