MADRID WABEBA TAJI LA TATU MFULULIZO UEFA BAADA YA KUILAZA LIVERPOOL 3-1
Timu ya Real Madrid imefanikiwa kuutwaa ubingwa michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya kwa kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Liverpool, mchezo ukipigwa nchini Ukraine.
Mabao ya Madrid yametiwa kimiani na Gareth Bale aliyefunga mawili pamoja na Karim Benzema. Bao pekee la Liverpool limetiwa kimiani na Sadio Mane.
Katika mchezo huo Liverpool walimtoa nyota wake Mmisri, Mohamed Salah baada ya kuumia Uwanjani wakati akiwania mpira na Nahodha wa Real Madrid, Sergio Ramos.
Ushindi huo wa Madrid unawapa taji la tatu mfululizo katika michuano hiyo na kuwafanya waweze kuweka historia ya aina yake tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
0 COMMENTS:
Post a Comment