May 28, 2018


Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Mohamed Hussein “Mmachinga’ amefunguka kuwa Yanga inahitaji kufanya marekebisho katika nafasi nne muhimu.

Nafasi hizo ni pamoja na namba tano, sita, tisa na 11 ambazo zimekuwa zikichezwa na wachezaji kama Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Thaban Kamusoko, Said Makapu na Obrey Chirwa.

“Yanga ilipambana kwa kiasi kikubwa lakini inatakiwa kufanyia kazi maeneo kadhaa ili kujiimarisha kwa ajili ya msimu ujao, kuongeza wachezaji wanacheza nafasi ya beki, kiungo, straika na winga,” alisema Mmachinga.

Kwa upande wa mshambuliaji wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe; “Yanga hawana namba sita mzuri, aliyepo umri umemtupa mkono hivyo anatakiwa mwenye uwezo, pia watafute kiungo mchezeshaji ambaye yupo imara hata winga wa mbele ambaye atakuwa msaada zaidi maana tangu aondoke Simon Msuva hakuna ambaye ameweza kuimudu nafasi yake.

CHANZO: CHAMPIONI


7 COMMENTS:

  1. ULIVYOANDIKA MASHINE NILIJUA LABDA YANGA WANATAKA KUANZISHA KIWANDA, SASA MASHINE HUKU KILICHOMO NDANI NI NAFASI ZA WACHEZAJI NI KUJITOA AKILI PAKUBWAAA

    ReplyDelete
  2. Tatizo ni mazoea yetu ya mfumo wa uchezaji. Tumezoea namba 7 na namba 11 wawe wachezaji wa kukimbia na mpira mbio za riadha. Mifumo ipo mingi.

    ReplyDelete
  3. huu uandishi gani,kama huna cha kuandika si ukae kimya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndivyo alivyo uyo niwale waliokua wanafurahia matatizo ktk yanga mchonganishi sana uyo

      Delete
  4. Ikiwa yanga imeshindwa kuwalipa mishahara yao wachezaji vipi wanatafuta mashine nne au hela ipo lakini sio ya mishahara ya walotowa jasho bali mashine mpya ndio muhimu zadi na sio za wakongwe. walioshindwa kutetea ubingwa?

    ReplyDelete
  5. Tatizo lako Saleh we we ni mnafki sana unaiponda sana yanga maandishi yako yakinafki mvuto umeupoteza ktk brog zako husipende kuelemea upande mmoja mpaka ukajulikana kama yule Mbolembole wa brog ya shafi dauda

    ReplyDelete
  6. Sahihi kabisa Mohammed Hussein mmachinga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic