May 26, 2018


Lechantre ambaye anaripotiwa kutokuwa na uhusiano mzuri na uongozi wa timu hiyo kutokana na kushinikiza kujua hatma yake, anatajwa miongoni mwa makocha walioom­ba kazi ya kuinoa Cameroon.

Kwa mujibu wa gazeti la Championi, Kocha huyo anadai kwamba mawakala wake ndio wamemuombea kazi hiyo Cam­eroon bila yeye kujua chochote, lakini uhakika ni kwamba ana­wasiliana nao kwa ukaribu zaidi na anawapa maelekezo muhimu na akinyanyuka anasepa na msaidizi wake.

Shirikisho la Soka la Cameroon limeham­ishia zoezi la usaili wa kocha mpya nchini Ufaransa ambapo jopo lilianza kazi Mei 19 na watamaliza ndani ya wiki mbili na Lechantre anatajwa miongoni mwa waliopita mchujo wa kwanza uliokuwa na makocha 70.

Habari zinasema kwamba kocha huyo huenda akatoweka nchini kurejea kwao kuwahi usaili huo wakati Simba ikimalizia mechi yake ya mwisho Jumatatu ijayo dhidi ya Majimaji inayopigana isishuke daraja.

Mfaransa huyo alitua Simba Januari, mwaka huu akipokea mikoba ya Mcameroon, Joseph Omog na ameifundisha timu hiyo mich­ezo 15 ya ligi kuu na kutwaa ubingwa wa ligi hiyo kwa kupoteza mchezo mmoja tu.

Lechantre alisaini mkataba wa miezi sita ndani ya Simba huku akiliambia Gazeti la France Football ya Ufaransa kwamba alikubali kusaini Simba kutokana na ushawishi wa mfanyabiashara mmoja mwanachama wa Simba ambaye alimhakikishia kwamba kuanzia mwezi ujao mambo yatakuwa sawa.

Inaelezwa kwamba sababu kubwa ya kocha huyo kutaka kuondoka ni dau la mshahara wa zaidi ya Sh milioni 20 kwa mwezi anaotaka am­bao hauendani na mapato halisi ya klabu hiyo.

Hata hivyo, jana Alhamisi wakati Simba ikikabidhiwa fedha zao kama mabingwa na wadhamini wao, Kampuni ya SportPesa, kocha huyo aliwasili katika eneo la tukio lakini al­itoweka ghafla bila kujulikana alipokwenda na hata viongozi walipoulizwa alipo walishangaa kutomuona.

“Siwezi kuzungumza kuhusu hilo kwa sasa,” alisema Said Tully ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Mashindano na mtu mwenye ush­awishi ndani ya kamati ya usajili.

Hata hivyo, taarifa baadaye zilisema kocha huyo na msaidizi wake, Mohammed Aymen walikwenda kuonana na Mwekezaji wa Simba, Mohammed Dewji ‘MO’.

Habari zinasema kwamba Dewji ambaye ameidhinishwa kuwekeza asilimia 49 Simba, bado haijaeleweka msimamo wake juu ya wataalam hao ingawa kwenye ishu ya msha­hara wanaotaka kila mmoja lazima wajadiliane kwa kirefu.

Taarifa zinasema, hivi sasa Simba imeanza mchakato wa kumtafuta mbadala wa Mfar­ansa huyo, lakini MO anaweza kumbakisha baada ya kuingilia kati suala hilo.

1 COMMENTS:

  1. Kwa kiasi fulani ni vigumu kufahamu Bongo ni taarifa gani ya habari imetolewa na udaku au chanzo makini cha habari cha kuaminika. Taarifa nyungi zinazotolewa zinavimelea vya udaku wa vyanzo vya habari visivyokuwa na uhakika na wanachohabarisha. Katika siku kadhaa hivi za karbuni tumekuwa tukihabarishwa habari inayomuhusu kocha wa SIMBA. Mara leo hivi mara kesho vile. Mara anaondoka, nara anachgua wachezaji wake wa msimu ujao, mara anlipwa pesa nyingi, mara anataka kuongezewa pesa zaidi,mara hawataki wachzaji fulani mara vile,kwa kweli mambo mengine ni ushuzi mtupu. Hatujawahi kumuona yeye mwenyewe kocha akitoa kauli yake au viongozi wa klabu yake wakithibitisha taarifa hizo. Kubwa kuliko yote SIMBA ya sasa ikiwa kweli inamuhitaji mfaransa kufanya nae kazi basi hakuna wasiwasi wote wanao uwezo wa kumuhudumia kocha huyo. Na kama SIMBA wataamua kuachana nae au yeye mwenyewe kocha akiamua kuondoka basi anaweza kufanya hivyo na SIMBA wakaleta kocha mkubwa zaidi kitaaluma zaidi yake au hata wakaamua kuendelea na Mrundi ni kocha mzuri tu. Ushauri kwa vyombo vyetu vya habari hasa za michezo vinatakiwa kujikita zaidi katika kuelimisha watanzania hasa kuhusiana na soka la ndani la bara la Africa kwa mfano kungekuwa na uchambuzi wa mara kwa mara wa kiuchunguzi kuhusiana na vilabu ambavyo mara nyingi vimekuwa vikwazo kwa timu zetu kusonga mbele kwenye mashindano ya Africa. Tusisubiri kwa timu zetu kuifahamu Almasry au cotton sports mpaka wakati wanapangwa kucheza nazo. Taarifa za habari za michezo zimejaa utajiri wa habari kuliko kujikita kunako udaku peke yake. Nnaimani zaidi kuwa Simba,Yanga au Azam wanaweza kuwa na kazi rahisi wakikutana na Manchester United kuliko wakikutana na Elhilali ya Sudani. Hakuna kijana wa kitanzania asiweza kukutajia kikosi cha Manchester United au Arsenal seuze kwa wachezaji wa Tanzania na hiyo yote ni kutokana na uhabarishaji uliotukuka kwa timu za ulaya kwa vyombo vyetu vya habari kwa timu za ulaya na nje ya Africa wakitelekeza kwa kiasi kikubwa habari za soka za ndani ya Africa. Wazungu waliamua kwenda mwezini baada ya kuimaster dunia lakini sisi Waafrica hasa watanzania tunahangaika kuumaster mwezi kabla hata kuyajua mazingira yanayotutawala.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic